Wagombea
katika nafasi mbalimbali za uchaguzi za Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) na wadau wa soka wamekatwa na TAKUKURU kwa tuhuma za
kujihusisha na rushwa jijini Mwanza.
Miongoni
mwa waliyokamatwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es
Salaam (DRFA), Almas Kasongo, Shafii Dauda ambaye pia ni Mtangazaji wa
Clouds Media Group, Elias Mwanjale, Leonald Malongo, Effam Majinge,
Osuri Kasuli, Richard Kayenzi, Lazack Juma pamoja na Kelvin Shevi.
Hayo
amebainisha Msemaji wa Takukuru Ernest Makale na kusema waliwakamata
watu hao kwa kuweka mitego sehemu wanazofanyia vikao vyao vya siri.
"Tumewakamata
kwa sababu hiki siyo kipindi cha kampeni na dalili zote kwamba walikuwa
hapa kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa zilikuwa zipo wazi, kama
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa tumeona kuna viashiria vya
rushwa, tukaweka mitego katika sehemu walizokuwa wanaendesha vikao vyao
vya siri tukaweza kuwakamata", amesema Makale.
Pamoja
na hayo Makale amesema watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana ila
wanaendelea na uchunguzi wao endapo watakapopata ushahidi wa kutosha
watafikishwa mahakamani.
0 comments:
Chapisha Maoni