Serikali
imesema kuwa imepunguza bei ya vifaa mbalimbali vinavyotumika katika
sekta ya afya zikiwemo bei za dawa, vitendea kazi na vifaa tiba vya
maabara vinavyonunuliwa na kusambazwa na Bohari ya Dawa(MSD) kwa
asilimia 15
Hayo
yamesmwa jana na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na
wafanyakazi wa Bahari ya Dawa (MSD) ambapo alisema kuwa hayo ni matokeo
ya utaratibu wa kuanza ununuzi wa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji
kama Rais Dkt. John Magufuli alivyoagiza.
Alisema
kuwa kwa sasa Halmashauri, Hospitali na Vituo vya Afya vianapaswa
kutumia bei elekezi ya dawa iliyotolewa na Wizara ya Afya ambayo ipo
kwenye kitabu ya orodha ya bei cha MSD.
“MSD
kwasasa inaagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji
wanchizipatazo 20 ambazonipamojana Kenya, Uganda, Afrika Kusini, India,
Bangladesh, Pakistan, Jamhuri ya Watu wa Korea, China, Ujerumani,
Uingereza, Uswisi, Denmark, Ufaransa, Ubelgiji, Italia, Romania,
Marekani, Cyprus, Falme za Kiarabu, na Tanzania,”alisema Ummy Mwalimu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema tayari
wametoa mikataba 73 kwa wazalishaji ambapo kati ya hiyo 46 ni ya
wazalishaji wa dawa ambao wanatoka nchi za Uganda, Denmark, Ufaransa,
Ujerumani, China, Afrika Kusini, Nchi za Falme za Kiarabu,Bangladesh,
India, Kenya na Tanzania ambao wanazalishia aina 178 za dawa.
Hata
hivyo, kwa upande wa vifaa tiba alisema jumla ya wazalishaji 18
wamepata mikataba ambao wanatoka Uingereza, Ujerumani, India, Kenya na
Tanzania, kwa ajili ya aina 195 za vifaa tiba.Aidha, kwa upande wa
vitendanishi vya maabara, jumla ya wazalishaji 9 kutoka nchi za
Uingereza, Ujerumani, Ubelgiji, Romania, China, India na Kenya wamepata
mikataba kwa ajili ya aina 178 za vitendanishi vya maabara.
0 comments:
Chapisha Maoni