Rais John Magufuli anazindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo wilayani Sengerema kesho.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,
Emmanuel Kipole alisema jana kuwa, Rais Magufuli atafika wilayani hapo
saa mbili kwa ajili ya uzinduzi huo.
Mradi
huo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2014 kwa gharama ya Sh23 bilioni
utawanufaisha zaidi ya wakazi wa wilaya hiyo zaidi ya 13,000.
“Lakini
akiwa njiani kuelekea katika tukio la kuzindua mradi huo atasalimiana
na wananchi barabarani kadri itakavyowezekana na baada ya kuzindua mradi
huo atawahutubia wananchi wa Sengerema na viunga vyake hivyo wananchi
wajitokeze kwa wingi,” alisema Kipole.
Kipole
alisema wilaya hiyo ina jumla ya wakazi 74,186 kutokana na Sensa ya
Watu na makazi ya mwaka 2002, hivyo mradi huo kwa sasa utahudumia kata
11.
Kata
hizo ni Sima, Nyatukala, Ibisabageni, Mwabaruhi, Nyampulukano, Misheni,
Tabaruka, Nyampande, Nyamazugu, Nyamazeze na Ibondo.
Mhandisi
wa Maji Wilaya ya Sengerema, Nikas Ligombi alisema mradi huo
uliofadhiliwa na Benki ya Afrika umekamilika kwa asilima 100 na
utakapozinduliwa rasmi tatizo la maji katika mji wa Sengerema litakuwa
limepatiwa ufumbuzi.
“Lita
za ujazo 150,000 zitakuwa zinasukumwa kila siku kutoka kwenye chanzo
cha maji kwenda kwenye matanki ya kusambaza mitaani,” alisema Ligombi.
Mkuregenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Sengerema, Magesa Mafuru alisema ni fahari
kubwa kukamlika kwa maradi huu ambao utamaliza matatizo ya maji
yaliyokuwa yakiukabili mji huo na kuwataka wananchi kuutunza na
kuuthamini ili udumu kwa muda mrefu.
Mmoja
wa wakazi wa mjini humo, Jumanne Kashiba alisema baada ya mradi huu
kukamilika tatizo la maji mjini hapo lilokuwa likiwakabili litakoma na
kuipongeza serikali kwa jitihada hizo.
0 comments:
Chapisha Maoni