test

Alhamisi, 20 Julai 2017

NRM kubadili katiba ili Kumwongezea muda Rais Museveni


Chama tawala nchini Uganda cha National Resistence Movement (NRM) kimeapa kuhakikisha kwamba katiba ya nchi hiyo ina badilishwa ili kumruhusu Rais Yoweri Museveni kuitawala Uganda hadi mwisho wa umri wake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa leo katika mtandao wa Idhaa ya Kiswahili VOA inaeleza kuwa, NRM,  imetangaza kutumia mbinu zote kuhakikisha kwamba katiba ya nchi inabadilishwa ili kumruhusu Rais Museveni kutawala hadi kifo chake. Hata hivyo Wanasiasa wa upinzani nao wameapa kuzima kila jaribio la kuifanyia katiba marekebisho.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, japokuwa Museveni amekaa kimya, viongozi wa NRM, wanasema wanasiasa wa upinzani wanamaliza muda wao kupinga nia ya chama tawala kuondoa ibara ya 102 B inayomzuia mtu yoyote aliyetimiza umri wa miaka 75 kuwania madaraka ya urais.

Viongozi hao wanaongozwa na mshauri wa Rais, David Mafabi ambaye amesema kuwa: “Hakuna wasiwasi kuhusu hilo. Tunataka katiba ibadilishwe na tunaieleza dunia ijue. wanaopinga wachunguze.

Kulingana na viongozi wa chama cha NRM, umri hauwezi kuwa kizuizi kwa kiongozi aliye na uwezo wa kuingoza nchi, na kwamba hakuna mtu yeyote nchini humo anayeweza kuwa rais isipokuwa Yoweri Kaguta Museveni.

Wanasiasa wa upinzani wakiongozwa na Dkt Kiiza Besigye wa FDC na Nobert Mao, kwa upande wao, wameendeleza kampeni ya kutaka raia kususia jaribio la serikali kuifanyia marekebisho katiba wakitishia kutumia mbinu zote kuzima hatua hiyo.

Katiba ya Uganda ilifanyiwa mabadiliko mnamo mwaka 2005 na kuondoa kizuizi cha mihula miwili, iliyomwezesha Museveni kuwania urais kwa mara nyingine. Museveni ameitawala Uganda tangu mwaka 1986.

Chanzo VOA Swahili

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni