SERIKALI
ya Norway imeipatia Tanzania msaada wa Dola Milioni 10.5 za Marekani
kupitia programu ya miaka mitatu ya maboresho ya Mamlaka ya Mapato
Tanzania, inayotarajiwa kuanza Mwaka Mpya wa Fedha- Julai Mosi mwaka
huu.
Mpango
huo pamoja na uzinduzi wa Awamu ya Pili ya Program ya Maendeleo ya
Sekta ya Mafuta, umezinduliwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya
Nje wa Norway Borge Brende, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip
Mpango na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Dkt.
Juliana Pallangyo kwa niaba ya Serikali zao.
Dkt.
Mpango ameishukuru Serikali ya Norway kwa msaada huo mkubwa
utakaochangia kuboresha utendajikazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa
kuijengea uwezo zaidi wa kitaalamu, miundombinu na vitendeakazi vingine
vitakavyo changia kuongeza uwezo wa Mamlaka hiyo wa kukusanya mapato ya
Serikali.
Kwa
upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi
Dkt. Juliana Pallangyo amesema kuwa hatua ya Serikali ya Norway
kuendelea kufadhili programu ya pili ya Mpango wa kuendeleza Sekta ya
Mafuta utaiwezesha Serikali kubobea katika masuala ya utaalamu wa
masuala ya sheria na usimamizi wa sekta hiyo.
Nae
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Mhe. Borge Brende amesifu utendaji
kazi mahili wa Mhe. Rais Dokta John Pombe Magufuli wa kupambana na
ufisadi na vitendo vya rushwa pamoja na kuimarisha ukusanyaji kodi,
hatua ambayo itaifanya nchi ipige hatua za maendeleo haraka.
Amesema
kuwa hajawahi kuona nchi yoyote duniani ikiendelea bila kuweka nidhamu
na uwajibikaji serikali pamoja na kutokusanya mapato yake ipasavyo na
kuahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na serikali ya awamu ya
tano kufanikisha mipango yake ya kuwaletea wananchi wake maendeleo.
0 comments:
Chapisha Maoni