Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema gurudumu la demokrasia limekwisha kuanza nchini hivyo ni vigumu kulizuia.
Lowassa
ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alirejea Makao Makuu
ya Polisi Dar es Salaam jana baada Juni 27 kuhojiwa na Ofisi ya
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
Alihojiwa
kwa takriban saa nne juu ya kauli alizozitoa kuhusu viongozi wa dini wa
kundi la Uamsho na akatakiwa kurudi jana saa 6.00 mchana.
Akizungumza
ofisini kwake Mikocheni, Lowassa alisema baada ya kuitikia wito wa
polisi jana, hakuna mengi aliyoambiwa zaidi ya kuelezwa kuwa upelelezi
wa suala hilo unaendelea hivyo arejee ofisini hapo Julai 13.
Alipoulizwa analichukuliaje suala hilo la kutakiwa kwenda polisi mara kwa mara alisema: “Njoo kesho, njoo kesho kutwa ni sehemu ya kazi yao (polisi).
“Kuhusu maoni yangu nitawaambia baada ya kumaliza hili, isionekana naingilia.
“Lakini nieleze jambo moja, demokrasia ikishaanza kuizuia ni taabu sana.
“Unaweza ukapunguza spidi ya gurudumu la demokrasia lakini huwezi kuiondoa, demokrsia imeshaanza, inaendelea, ni vigumu kuizuia.
“La
pili, nichukue nafasi hii kuwaomba wanachama wa chama chetu na wananchi
na wanaotutakia mema wasiwe na shaka kila kitu kipo chini ya utaratibu
mzuri.
“Tuko
sawasawa, tuko sahihi na tunatekeleza kama alivyosema (Mwenyekiti
Chadema, Freeman Mbowe). Tunatekeleza sera ya chama chetu, wasiogope
wawe na amani, watulie,” alisema Lowassa.
Alivyoulizwa kama wakati anatoa kauli kuhusu viongozi hao wa Uamsho labda aliteleza, Lowassa alisema, “I stand by what I said” (naisimamia kauli yangu).
Alisema anaamini alichosema ni sahihi kama alivyoeleza Mbowe na kwamba suala la msingi ni kuachiwa kwa Masheikh wa Uamsho.
Lowassa
alisema Chadema kama chama hakisemi kama viongozi hao wa dini wana
makosa ama hawana, ila wamekaa ndani kwa muda mrefu bila kesi zao
kusikilizwa.
“Wamekaa
vya kutosha, hilo ndilo la msingi tunaloomba… katika hotuba yangu
nilisema na kwenye magazeti waliandika vizuri, wale walioko madarakani
wana mamlaka.
“Mtu mwenye dhamana ya kuwatoa ni Rais. Nikawaeleza wajipange wakaongee na Rais wamwambie ‘mzee, wenzetu tunaomba waachiliwe’.
“Mwenye
madaraka ya mwisho ni Rais, mkiendelea na mahakama miaka minne, nane
siyo… kwa hiyo narudia, ni vema wakamuombe Rais awaachilie.
“Sintoshangaa
akitekeleza (akawaachia) kwa sababu juzi ametekeleza moja ya uamuzi
wetu wa kuunda tume ya kuchunguza madini, tulivyokuwa Kahama tulisema
tutaunda tume.
“Waendelee na uchunguzi wao (juu ya kauli yake), lakini narudia, gurudumu la demokrasia likianza kulizuia ni taabu sana.
“Narudia mwenye mamlaka ya mwisho kuombwa na kushawishiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”alisema Lowassa.
0 comments:
Chapisha Maoni