Kiongozi
wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un amemkejeli Rais wa Marekani, Donald
Trump saa chache baada ya kufyatua kombora zito ambalo linadaiwa kuwa na
uwezo wa kufika Alaska Marekani na sehemu nyingine duniani.
Timu
ya ujasusi ya Marekani ilieleza kuwa kombora hilo la Korea Kaskazini
lililofyatuliwa wiki hii limeonesha kufanikiwa kwa kiasi kikubwa na
kwamba lilienda umbali wa zaidi ya Kilometa 900 kabla halijatua baharini
kwenye eneo muhimu la kiuchumi nchini Japan.
Kwa
mujibu wa Sky News, Kim Jong-Un ameeleza kuwa kombora hilo
lililofyatuliwa Julai 4, siku ya kuadhimisha uhuru wa Marekani, lilikuwa
zawadi yake kwa Marekani na kiongozi wake.
“Lilikuwa lenye muonekano wenye mvuto kama mvulana mtanashati,” Sky News inamkariri Kim Jong-Un. “Ilikuwa zawadi nzuri kwa Marekani siku ya maadhimisho ya uhuru wao,” anadaiwa kuongeza.
Taarifa
iliyotolewa na Ikulu ya Marekani imeeleza kuwa Rais Trump na timu ya
wana usalama inaendelea kuvifanyia usaili wa karibu vitendo vya Korea
Kaskazini na kwamba nchi hiyo imefikia ukomo wa uvumilivu wake.
Imeeleza
kuwa Marekani itaongeza vikwazo zaidi dhidi ya nchi hiyo wakati ambapo
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kujadili hatua dhidi
ya Korea Kaskazini.
Urusi
na China, jana zilitoa tamko la kulaani majaribio ya makombora
yanayofanywa na Korea Kaskazini, ambayo ni tishio kwa dunia nzima.
Kombora
hilo aina ya Hwasong -14 liliruka umbali wa kilomita 2,802 na kusafiri
kwa umbali wa kilomita 933 kwa dakika 39 kabla ya kuanguka baharini.
Korea Kaskazini imesema kuwa ni taifa lililojihami kinyuklia ambalo linamiliki kombora la masafa marefu linaloweza kushambulia eneno lolote duniani
Korea Kaskazini imesema kuwa ni taifa lililojihami kinyuklia ambalo linamiliki kombora la masafa marefu linaloweza kushambulia eneno lolote duniani
0 comments:
Chapisha Maoni