Saa
chache baada ya bunge kipitisha sheria ya marekenisho ya sheria
mbalimbali itayayoleta mageuzi makubwa katika usimamizi wa rasilimali za
taifa, kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia imemtaarifu msuluhishi
kuhusu uwepo wa mgogoro kati yake na serikali ya Tanzania.
Serikali
iliwasilisha bungeni miswada mitatu inayohusu rasilimali za taifa
ambayo ina lengo la kubadili sheria zinazosimamia madini sasa nchini
kufuatia kubainika kuwa taifa linapoteza mabilioni ya fedha kila mwaka
kupitia sekta ya madini.
Baadhi
ya mapinduzi yatakayoletwa na sheria hizo ni pamoja na Benki Kuu ya
Tanzania kupewa mamlaka ya kuhifadhi dhahabu baada ya kutokufanya hivyo
kwa miaka mingi, huku sheria ikitamka kuwa madini ni mali ya watanzania
wote kupitia kwa rais wa nchi.
Sheria
hizo zitaiwezesha serikali kufanya uangalizi wa maeneo ya uchimbaji wa
madini huku ikihakikisha hakuna ndege itakayotua na kuondoka na madini
kama ilivyokuwa awali.
Kufuatia
mabadiliko hayo, Acacia jana ilitoa taarifa kuwa Kampuni ya Bulyanhulu
Gold Mine (BGM) na Pangea Mineral Limited (PML) zimetoa notisi ya
usuluhishi kufuatia uzuiwaji wa usafirishaji wa mchanga wa madini.
Taarifa
hiyo iliyochapishwa katika tovuti rasmi ya Acacia ilieleza kuwa, notisi
hizo zinarejea mgogoro wa sasa na serikali ya Tanzania dhidi ya BGM NA
PML kwenda katika usuluhishi.
Japo
kuwa Acacia hawakueleza wamefungua wapi amombi hayo ya usuluhishi
lakini walieleza kufanya hivyo kwa wakati huu ni jambo muhimu ili
kulinda kampuni wakaeleza pia majadiliano ndio njia bora itakayosaidia
kuleta maafikiano ambapo wakati huo wote wao wateendelea kufanya kazi
Tanzania.
Wakati
majadiliano ya usuluhisi yatakapoanza, Acacia hawatakuwa sehemu ya
majadiliano hayo yatakayofanyika kati ya Tanzania na Barrick Gold ambao
ndio wamiliki wakubwa wa Acacia.
Aidha wamesema kuwa maafikiano yoyote yatakayofikiwa katika majadiliano hayo yatatakiwa kuridhiwa na Acacia na kwamba watatoa ushirikiano kwa Barrick wakati wa mazungumzo.
Aidha wamesema kuwa maafikiano yoyote yatakayofikiwa katika majadiliano hayo yatatakiwa kuridhiwa na Acacia na kwamba watatoa ushirikiano kwa Barrick wakati wa mazungumzo.
Acacia
walisema kuwa mgodi yake mitatu inaendelea na uchimbaji kwa kutumia
makubaliano ya awali na kwamba itaendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu
yatakayojiri pamoja na miswada iliyopitishwa na bunge la Tanzania.
0 comments:
Chapisha Maoni