KWA kuonyesha ni kumpa dongo mpenzi
wake wa zamani, staa mwenye mvuto wa kipekee Bongo Muvi, Jacqueline
Wolper amesema kuwa katu hawezi kumuweka hadharani mpenzi wake mpya kwa
kuogopa kuibiwa tena na wazungu.
Staa huyo alituma dongo hilo kupitia
mtandao wake wa Snapchat, ambapo alikuwa akisema kuwa, anatamani sana
kumuweka hadharani mpenzi wake huyo mpya lakini anaogopa kunyakuliwa
tena na wakware wa kizungu kama alivyofanyiwa kwa mpenzi wake aliyepita
ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva.
Star Mix hili lilimtafuta Wolper
ambaye baada ya kubanwa kutaka kujua jina la bwana huyo aliyenaye
alianza kwa kuangua kicheko na kusema kuwa kuna wakati mwingine mtu
anazungumza kufurahisha watu wacheke lakini si kwamba kuna mtu kweli kwa
sasa.
“Jamani kuna kipindi mtu unawafanya watu wafurahi na kucheka sio kila unachozungumza mtu kiwe cha kweli.”
0 comments:
Chapisha Maoni