Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wake,
Humphrey Polepole kimetangaza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu
nchini ambao wamekosa mikopo ya kuendelea na masomo na wanafunzi ambao
ni yatima.
Taarifa
iliyotolewa na Polepole inasema kuwa wanafunzi hao wanapswa kufika
katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili
waweze kusaidiwa shida zao hizo za mikopo, jambo ambalo limepokewa
tofauti na baadhi ya watu wakidai kuwa suala la kutoa mikopo kwa
wanafunzi ni jukumu la bodi ya mikopo.
Kutokana
na mitazamo ya watu kuwa tofauti katika jambo hili, Humphery Polepole
aliibuka na kusema kuwa upinzani wa Tanzania ni mtihani mkubwa kwani
wanapojaribu kutatua matatizo ya watu wanakujua juu na wasipotatua
matatizo pia wanakuja juu.
"Tukikaa
kimya kwa shida za watu inakuwa tatizo, tukishughulika na shida za watu
inakuwa tatizo kubwa. Huu upinzani mtihani" alisema Polepole
0 comments:
Chapisha Maoni