test

Ijumaa, 2 Juni 2017

Wema Sepetu abadilishiwa mashtaka katika kesi ya dawa za kulevya


Msanii wa filamu nchini na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu jana alisomewa upya mashtaka katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili yeye na wenzake pamoja na maelezo ya awali.

Wakili wa serikali, Constatine Kakula mbele wa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba alisema kuwa kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa kwa maelezo ya awali lakini aliomba kufanya mabadiliko katika hati ya mashtaka, ombi ambalo lilikubaliwa na hakimu hiyo.

Wakisomewa mashtaka upya, Wema Sepetu na wenzake wanakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kukutwa na kiasi kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa hizo.

Wakili wa serikali alidai kuwa Februari 4 mwaka huu katika makazi ya msanii huyo eneo la Kunduchi, Ununio walikuta msokoto mmoja wa bangi na vipisi vyenye uzito wa gramu 1.08. Aidha, Wema anatuhumiwa kuwa, Februari Mosi katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya bangi.

Watuhumiwa wakikana mashtaka yote na wakili wa serikali akawasomea maelezo ya awali. Katika maelezo hayo, wakili huyo anasema baada ya vitu hivyo kupatikana vilipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kubainika kuwa ni bangi. Lakini pia Februari 8 Wema alipelekwa kwa mkemia na aligundulika kutumia bangi.

Wengine wanaoshtakiwa na Wema Sepetu ni wafanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa, Matrida Seleman Abbas ambao nao walikubali sehemu tu ya maelezo ya awali na kukana shtaka linalowakabili. Katika kesi hiyo, Wema Sepetu na wenzake wanatetewa na Wakili Peter Kibatala.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 14 mwaka huu.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni