Waziri
Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika amefunguka na kumshauri Rais
Magufuli jana bungeni na kusema Rais kabla ya kufikiria kuhusu makinikia
alipaswa kufikiria kuhusu madini yanayochimbwa na kuchenjuliwa pasipo
nchi kupata mapato.
Mnyika
alisema hayo jana bungeni wakati akichangia katika bajeti ya Wizara ya
Nishati na Madini ambayo imewasilisha makadirio ya mapato na matumizi
kwa mwaka wa fedha 2017/18 ambapo Waziri aliomba bunge liweze
kuidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 998. 3 ili kutekeleza majukumu
yake katika wizara hiyo.
"Rais
kabla ya kufikiria makinikia, angefikiria kuhusu madini yanayochimbwa
na kuchenjuliwa kwa ukamilifu hapa nchini lakini nchi haipati mapato
yanayostahili" alisema John Mnyika
Lakini
pia Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Madini ya Nishati na Madini, Dotto
Mashaka Biteko aliitaka serikali kufuta leseni zote za madini ambazo
hazifuati sheria na zinakiuka sheria ya madini na hazijatekelezwa kwa
muda mrefu ili wapewe wachimbaji wadogo wadogo.
"Leseni
zote ambazo zinakiuka sheria ya madini ikiwa pamoja na kutotekelezwa
kwa muda mrefu zifutwe na kupewa wachimbaji wadogo wadogo na wachimbaji
wa kati kwa kuwa wameonyesha nia ya dhati ya kuendeleza sekta hiyo"
alisema Biteko
0 comments:
Chapisha Maoni