Ikiwa
imepita siku mbili tangu Rais John Magufuli kueleza kuwa kwa sasa nchi
iko katika vita ya uchumi na kwamba ana majina ya watu waliotaka
kuingilia na kuharibu uchunguzi wa Kamati Maalumu aliyoiunda ili
kuchunguza thamani na viwango vya madini vilivyomo kwenye mchanga wenye
madini (Makinikia) katika makontena 277 yaliyozuiliwa kusafirishwa nje
ya nchi, ili kupoteza ushahidi.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole Mei 25, 2017 aliibuka na
kudai kuwa kuna wahujumu uchumi walitaka kumhonga kiasi cha Bilioni 300
Rais Magufuli, ili kusitisha zoezi la uchunguzi huo, huku akihoji
masilahi wanayopata watu wanaofanya biashara ya kusafirisha makinikia
hayo nje ya nchi.
“Vita
ziko za aina nyingi, ziko zile tunazopigana kwa silaha mtu na mtu, na
nchi na nchi, lakini sasa ziko vita za kiuchumi, ni mbaya zaidi
zinalenga kuturudisha nyuma.Wahujumu uchumi hawapigani na rais, bali
wanapigana na maisha ya wananchi wa Tanzania, tukiwa wamoja tutashinda
vita hii, wako watu wanaipinga vita hii yenye dhamira njema, huu si
wakati wa kutofautiana ni wakati wa kusimama kumshinda adui,” alisema.
Polepole
aliyasema hayo, wakati akitoa wito kwa wananchi, kumuunga mkono Rais
Magufuli katika kipindi hiki kigumu kwani nchi iko katika vita mbaya ya
uchumi ambayo wahujumu uchumi wamelenga kupigana na maisha ya watanzania
na kurudisha nyuma maendeleo ya Taifa.
“Kuna
watu walitaka kumhonga rais bilioni 300 ili kusitisha uchunguzi.
Walitaka kuhonga bilioni 300 kwa ajili ya kusitisha uchunguzi huo, hivi
wao wanapata fedha kiasi gani? Lakini rais akawatolea nje, akasema
subirini uchunguzi ukamilike. Tusiamame naye na hakika tutashinda na
historia itaandikwa kwamba tulisimama katika kulinda urithi wetu,” amesema.
Katika
hatua nyingine, Polepole aliwajibu baadhi ya wanansiasa wanaoikosoa CCM
kutokana na viongozi wake waliopita kutunga na kupitisha sheria za
madini ambazo zinatetea masilahi ya wawekezaji kuliko nchi, kwa kusema
kuwa viongozi walioko sasa ni tofauti na waliopita, na kwamba serikali
iliyoko madaraka itarekebisha sheria hizo.
“Tumehujumiwa
sana, tumedhurumiwa sana mali za watanzania ambazo tumezirithi kutoka
kwa mababu zetu na tuna dhamana ya kuhakikisha zinawafikia watoto wa
watoto wetu,” alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni