Mbunge
wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alihoji bungeni sababu za
wanafunzi wa CCM kupendelewa kufanya mikutano na sherehe za kumaliza
masomo yao huku wanafunzi wa vyama vingine vya upinzani hasa CHADEMA
kupigwa marufuku kufanya sherehe hizo.
Akijibu
jambo hilo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema
kuwa wanafunzi wa Chama Cha Mapinduzi huwa wanafuata utaratibu ndiyo
maana huwa wanapewa ruksa kufanya sherehe hizo pindi wanapomaliza vyuo
na kusema hao wengine huwa hawafuati utaratibu ndiyo maana wanakuwa
wanazuiliwa.
"Taratibu
ziko wazi kama CCM walikuwa wamefuata utaratibu na kupewa mikutano,
chama kingine chochote kinachotakiwa ni kufuata utaratibu zile zile
waweze kupewa mikutano lakini wengine kama hawajafanya utaratibu
hawatapewa tu kwa sababu CCM walipewa bali watapewa kwa kufuata
utaratibu, kuna sehemu zingine CHASO hao hao wamepewa mikutano kwa hiyo
linalotakiwa ni utaratibu tu wa kupewa mikutano hiyo" alisema Mwigulu Nchemba
Mbali
na hilo Waziri Mwigulu Nchemba alisema mikutano ya hadhara haijazuiwa
bali imewekewa utaratibu na kusema duniani kote sifa za mikutano ya
hadhara ni kama ambavyo inafanyika hivi sasa Tanzania na kusema kuwa mtu
aliyeshinda ndiye anaendelea na majukumu ya kuongoza na aliyeshindwa
hapaswi kushukuru kwa wananchi.
"Marekani
mwaka jana walifanya uchaguzi mmemuona Hillary Clinton anashukuru kwa
wananchi? Duniani kote aliyeshinda ndiye anaendesha serikali kwa
utaratibu wa kiserikali hili liko wazi duniani kote" alisisitiza Mwigulu Nchemba
0 comments:
Chapisha Maoni