Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema atatuma mkaguzi aende kuchunguza hali ya
upatikanaji wa dawa kwenye zahanati na kituo cha afya cha mjini Gairo,
mkoani Morogoro.
Kauli
hiyo aliitoa jana wakati akiwahutubia wakazi wa mji wa Gairo na
vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya
Shule ya Msingi Gairo ‘A’.
Waziri
Mkuu alifikia uamuzi huo baada ya kumhoji Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo,
Dk. Albert Lyaruu kama anamiliki duka la dawa au laa na kujibiwa kwamba
hana duka la dawa ingawa alikiri kwamba baadhi ya watumishi wa idara
yake wanayo maduka ya dawa.
“Sasa
ni lazima nilete mkaguzi kutoka ofisi yangu ili tupate picha halisi
kama dawa zinazoletwa zinafika, na kama zinafika zinatumikaje. Huyu
mkaguzi atakuja kukukagua wewe mwenyewe na kwenye zahanati zako.
“Kwenye
mkutano wangu na watumishi wa Serikali nimewaeleza kwamba ninyi ni desk
officers (maofisa wa kukaa ofisini tu), wala hamuendi vijijini kuona
hali halisi ikoje. Ndiyo maana wananchi hawa wanalalamikia kukosa dawa
na wewe wala hujui,” alisema Majaliwa.
Pamoja
na hali hiyo alimtaka mganga huyo kuhakikisha anakwenda kwenye vituo
vya afya na zahanati ili kuangalia matumizi ya dawa na kama hatofanya
hivyo anaweza kupata kesi kama ya Mkoa wa Shinyanga ambapo mganga wa
kituo cha afya alikutwa na dawa za Serikali nyumbani kwake, baada ya
wanachi kumwekea mtego hadi akakamatwa.
“Serikali
haizuii watumishi kuwa na maduka ya dawa, tunachokataa sisi ni kuchukua
dawa za Serikali ambazo zinatakiwa kuwatibu wananchi na kuzipeleka
kwenye maduka yenu. Tumezuia pia kuwepo kwa maduka ya watu binafsi nje
ya hospitali, zahanati au kituo cha afya,” alisema
Waziri
Mkuu aliwataka wananchi wa Gairo wawe macho na walinde mali za umma na
inapobidi watoe taarifa mara tu wanapobaini kuna mtu anatumia mali ya
umma vibaya.
Waziri
Mkuu alikuwa alimwita jukwaani, Dk. Lyaruu ili aeleze ni kiasi gani cha
fedha amepokea kutoka Serikalini kwa ajili ya ununuzi wa dawa na
alipotoa mchanganuo wake, wananchi waliohudhuria mkutano huo walizomea
na kudai kuwa siyo kweli.
“Ninapokea
shilingi milioni 109 kila robo mwaka. Na katika kipindi cha miezi
mitatu ya mwisho tumepokea shilingi milioni 109 na kati ya hizo tunatoa
asilimia 33 ambazo ni sawa na shilingi milioni 36 kununua dawa na vifaa
tiba. Kwa hiyo hadi sasa hali ya dawa ni nzuri na upatikanaji wake ni
kati ya asilimia 85 hadi 90,” alisema Dk. Lyaruu.
Kutokana na majibu yake hayo, wananchi walimzomea daktari huyo na kudai kuwa wananunua dawa hizo kwenye maduka ya dawa.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi waliohudhuria
mkutano huo kwamba dawa zinazopatikana kwenye zahanati zinatofautiana
na dawa zinazopelekwa kwenye kituo cha afya, hospitali ya wilaya au ya
mkoa.
0 comments:
Chapisha Maoni