Rais
Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefunguka na kusema
suala la kuongoza nchi ni kazi kubwa mno na kusema yeye toka amestaafu
kazi hiyo saizi anaweza kulala na usingizi ukaisha vizuri lakini kipindi
cha nyuma haikuwa hivyo.
Kikwete
amesema hayo jana kwenye Futari maalumu iliyoandaliwa na Kampuni ya
simu za mkononi nyumbani kwake Msoga, Pwani na kusema saizi mzigo huo
ameubeba Rais Magufuli na kudai huwa anamtia moyo kuwa anapaswa
kupambana kwani hata wao wamepitia mambo ambayo yeye anapitia.
"Sasa
nimestaafu muda wa kuwasaidieni ninao tofauti na zamani, zamani mambo
mengi kubeba mzigo wa kuongoza nchi kazi kubwa sana saizi anahangaika
nao Rais Magufuli wakati mwingine nampa moyo tu bwana wewe pambana,
wenzako wote ndiyo hivyo hivyo tulipitia humo humo pale unapodhani
unatenda jema asubuhi wanakuponda, ndiyo muziki wenyewe lakini mara kuna
hili kuna lile saizi mimi nalala usingizi unaisha kabisa kama kuna watu
wananisumbua watakuwa ni wajukuu tu" alisema Kikwete
0 comments:
Chapisha Maoni