Jumatatu
hii, Majaliwa alipiga marufuku usafirishaji wa mahindi alipokuwa mkoani
humo kwa ajili ya sherehe za Sikukuu ya Eid el Fitr.
Baada
ya agizo hilo, malori hayo yalikamatwa na kuzuiwa. Akijibu maswali ya
papo kwa papo bungeni leo ( Alhamisi) juu ya zuio hilo, Waziri Mkuu
amesema uamuzi huo ni moja ya hatua za kuhakikisha Taifa linajihadhari
na ukosefu wa chakula hasa ikizingatiwa kwamba kulikuwa na uhaba wa mvua
mwaka jana.
"Nampongeza Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama kwa kuyazuia malori hayo," amesema Majaliwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana Jumatano, Mghwira alisema
magari hayo yalikamatiwa eneo la Himo huku akipiga marufuku
usafirishwaji wa nafaka pamoja na sukari kwenda nchi jirani bila ya kuwa
na kibali maalumu.
“Baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakisafirisha sukari na nafaka nyakati za usiku huku wakishirikiana na baadhi ya askari polisi ambao si waaminifu, ni vema askari hao wakaacha mara moja kwani ni kinyume cha maadili ya kazi zao,”alisema mkuu huyo wa mkoa.

0 comments:
Chapisha Maoni