Vigogo
waliotajwa katika ripoti ya pili ya kuchunguza makontena yenye mchanga
wa madini (makinikia) kuisababishia Serikali hasara ya matrilioni ya
fedha kupitia sekta ya madini, walipokuwa wakihudumu katika nyadhifa zao
serikalini wamevunja ukimya.
Vigogo
hao wamezungumzia ripoti hiyo ya pili iliyowasilishwa kwa Rais Dk. John
Magufuli Ikulu Dar es Salaam jana, ambapo kamati husika ilichunguza
hasara ambayo nchi imepata tangu 1998 usafirishaji wa mchanga wa dhahabu
nje ya nchi ulipoanza.
Mbunge
wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM), alipoulizwa maoni yake juu ya kutajwa
na kamati hiyo, alisema hataki kuzungumza chochote juu ya ripoti hiyo,
huku Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja (CCM), akisema sheria ya
madini ya 2010 ingefuatwa, nchi isingekuwa hapa ilipo.
Kwa
upande wake Kamishna wa Madini wa zamani, Dk. Dalaly Kafumu, alisema
kwa sasa hawezi kuzungumza jambo lolote kwa kuwa na yeye ni mmoja wa
watuhumiwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo.
Baada
ya kutoka kwenye kipindi cha asubuhi cha Bunge ambacho alikuwa
akikiendesha, Chenge alipotakiwa kuzungumzia ripoti hiyo, alijibu kwa
ufupi.
“Sizungumzi na mtu,” na alipoulizwa kama hata salamu hataki, alisema. “Sizungumzi na mtu mimi,” alisema Change ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Chenge
alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kati ya 1972 na 1990, ambapo
mwaka 1993 aliteuliwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan
Mwinyi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali nafasi ambayo alidumu nayo hadi
mwaka 2005.
Mbunge
wa Igunga, Dk. Dalaly Kafumu (CCM), ambaye ametajwa kutaka kuingilia
ripoti ya kamati ya kwanza iliyochunguza mchanga huo, alisema hataki
kuzungumza chochote kwa sasa ingawa anaamini kila kitu kiko sawa.
“Kwa
kuwa nimetajwa kama mtuhumiwa, sitaki kusema kitu kwa sasa kwa sababu
hili ni sawa na jambo lililo mahakamani tu kwa kuwa wamesema tutahojiwa,
lakini kila kitu kiko sawa,” alisema Dk. Kafumu.
Alipoulizwa
kama ni kweli alikutana na Profesa Abdulkarim Mruma, aliyekuwa
mwenyekiti wa kamati hiyo ya kwanza na ni nini walichozungumza, Dk.
Kafumu alisema. “Nimeshasema no comment (sina la kusema ),” alisema Dk. Kafumu.
Dk.
Kafumu ni moja ya watumishi waliohudumu ndani ya Wizara ya Nishati na
Madini ambapo alifanyakazi kazi ndani ya wizara hiyo kuanzia mwaka 1983
hadi 2011, alipoacha na kwenda kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa
marudio wa Igunga, baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo
Rostam Aziz.
Taarifa
zilizopo kwenye tovuti ya Bunge zinaonesha, mwaka 1983 mpaka 1987, Dk.
Kafumu alikuwa mtaalamu wa miamba na madini wa wizara hiyo, mwaka 1987
mpaka 1992, mkufunzi na mtafiti wa madini, mwaka 1992 mpaka 2002 akawa
mtaalamu mwandamizi wa madini, mwaka 2002-2004, mtaalamu wa miamba mkuu
na mbobezi wa madini, mwaka 2004-2006, alikuwa ofisa mawasiliano na
mwaka 2006 mpaka 2011, alikuwa kamishna wa madini.
Kwa
upande wake Ngeleja aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, kuanzia
mwaka 2008 hadi 2012, alisema hataki kuzungumzia juu ya kilichoelezwa na
kamati hiyo ikiwamo kutajwa kwake, bali anachoweza kusema ni kuwa, Rais
Magufuli ameonesha uzalendo.
“Sitaki
kuzungumza yaliyo kwenye ripoti ya uchunguzi, ila tu nisema kwa wale
tuliosikiliza wakati ripoti inawasilishwa na wakati Rais mwenyewe
anazungumza, unaona hisia za uzalendo ambazo Rais anazo, na ameeleza kwa
uchungu mkubwa namna ambavyo tunastahili kupata zaidi kuliko
tunachopata sasa.
“Lakini
jambo kubwa alilolifanya, amesema atamkabidhi taarifa (Spika wa Bunge),
kwa sababu msingi wa mambo yote haya ni sera na sheria za nchi.
“Kwamba
sisi kama Bunge tutimize wajibu wetu tuhakikishe mapungufun yote yaliyo
pale tunayafanyia kazi, lakini kikubwa amesema chenji (fedha
zilizokwepwa na migoni) yetu irudi na amewakaribisha wawekezaji wakae
mezani, lakini baada ya kuzingatia masilahi ya upande wetu, ni jambo
jema.
“…wakati
nachangia bajeti ya Wizara ya Nishati nilisema, sheria hata tuliyo nayo
sasa tungekuwa tumeitekeleza vizuri tusingekuwa hapa tulipo na moja ni
kuhusu mikataba iliyofungwa kabla ya mwaka 2010,” alisema
Alisema
kifungu cha 116 cha Sheria ya Madini, kinasema mikataba yote
iliyofungwa kabla ya kutungwa kwa sheria ya madini ya mwaka 2010,
inatakiwa iheshimu na itambulike kwa utaratibu wa sheria hiyo.
“Kwenye
kifungu cha 11 cha hii sheria ya madini, inasema kila baada ya miaka
mitano baada ya kuanza kutumika hii sheria, mikataba yote ya madini
ipitiwe upya.
“Mimi
nilijiuzulu uwaziri Mei 4, 2012, sasa ni miaka mitano imepita, na
wakati najiuzulu mimi tulikuwa tumemaliza kutunga kanuni, ninachotaka
kusema ni kwamba kupitia hicho kifungu cha 11 hilo ndilo dirisha la
kujadiliana yale ambayo kipindi kile kilishindikana,” alisema
Waziri
huyo wa Nishati na Madini wa zamani, alisema kuwa kifungu cha 10 cha
sheria hiyo kimeweka wazi namna Serikali inavyoweza kumiliki hisa
kimkakati kwa kutumia dirisha hilo.
“Utaratibu
huo ndiyo tumeutumia kwa Mchuchuma na Liganga, ambapo serikali ina
asilimia 20 za bure, Ngaka ina asilimia 30 za bure, hayo ndiyo
niliyosema,” alisema Ngeleja.
0 comments:
Chapisha Maoni