Rais John Magufuli amemtaka Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Archado Mtalemwa ajiandae kustaafu kutokana na mapungufu mengi ambayo Rais amesema ameyaona katika mamlaka hiyo.
Rais
ameyasema hayo leo(Jumatano) akiwa katika ziara yake ya siku tatu
mkoani Pwani na alitumia fursa hiyo kuzungumzia miradi ya maji na
ulipaji wa maji kwa taasisi za serikali.
“Ndugu
yangu Mtalemwa, naongea kwa lugha nzuri hapa, nikuombe tu kuwa ustaafu
mapema, inawezekana Waziri wa Maji ni rafiki yako, kama ilivyo kwa
mawaziri wengine, lakini nadhani huu ni wakati mzuri,” amesema na kuongeza;
“Pamoja na kazi zako nzuri, it’s your time to go.”
Rais Magufuli amezungumzia kero mbalimbali za maji na kusema kuna upotevu mkubwa wa maji.
0 comments:
Chapisha Maoni