
Raisi John Magufuli amesema kuna pembejeo hewa kama ilivyo kwa watumishi na wanafunzi hewa.
Akizungumza
leo (Jumatano) wakati akizindua kiwanda cha chuma cha kuunganisha
matrekta cha Ursus, Rais Magufuli amesema tatizo la pembejeo hewa ni
kubwa na sasa analifanyia kazi na muda wowote ataliweka hadharani.
Amesema
amebaini katika mpango wa kusambaza pembejeo nchini wapo wakulima
walioandikishwa majina yao lakini kumbe walishafariki zaidi ya miaka 20
iliyopita na wengine wanaodaiwa kusambaziwa kumbe hata si wakulima na
hawana hata mashamba.
Rais amesema hayo katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani.
Amesema
tayari ameipa kazi timu maalumu ya watu kufanya uchunguzi wa kina
kuhusu pembejeo hewa ambazo amedai ni nyingi na akiikamilisha ataanika
hadharani madudu hayo na wahusika wote watashughulikiwa.
“Yaani
hata kwenye pembejeo nimebaini zipo hewa, majina ya watu unakuta ni mtu
aliyefariki miaka zaidi ya 20 iliyopita, mengine mtu hana hata shamba
sasa kila kitu ilikua hewa, na hapa naamini tatizo ni kubwa lakini
tutalimaliza kama lile la wanafunzi na watumishi, wapo watu wanafanya
hii kazi ikikamilika tu tutaeleza,"amesema
Rais
amesema asilimia 80 ya Tanzania inategemea kilimo lakini eneo hilo
halina maendeleo kwa sababu wengi wanatumia jembe la mkono.
Lakini kama wakianza kutumia matrekta basi kilimo chetu nchini kitakua cha tija kwani wakulima wengi watazalisha zaidi.
Ameitaka
Wizara ya viwanda na uwekezaji, wizara ya kilimo na wawekezaji wa
matreta hayo waangalie suala la bei ili isiwe kubwa na kuwafanya watu
kushindwa kuyanunua.
Katika
ziara yake amelitaka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) wabadiliie
katika utendaji kazi sababu huko nyuma kila kilichokua kibaya akiuliza
imetajwa NDC hadi akawa ameanza kutaka kufumua lakini kupitia ziara hiyo
ameona mabadiliko mengi yenye tija kwenye uanzishwaji viwanda hivyo
vitatu alivyotembelea Kibaha.
0 comments:
Chapisha Maoni