Mbunge
wa Nkasi (CCM), Ally Kessy amefunguka na kusema watu waliohusika
kusaini mikataba mibovu ya madini wanatakiwa kunyongwa kwani nchi
ikitapoteza watu ishirini au thelathini hakuna hasara yoyote.
Mbunge
Kessy anasema kama watu hao waliotia saini ya mikataba ya madini mwaka
1998 watakamatwa na mali zao kunyang'anywa na wakanyongwa itakuwa ni
fundisho kubwa kwa watu wengine na baadhi ya wabunge wengine waliunga
mkono hoja hiyo huku wakitaka mikataba hiyo ya madini iweze kupitiwa
upya.
"Wakamatwe
wote waliohusika na mikataba mibovu na kusababisha kuingizia serikali
hasara, ikiwezekana wanyongwe hata ishirini au thelathini maana nchi hii
wanazaliwa watu Muhimbili zaidi ya mia moja kwa siku, Bungando
wanazaliwa mpaka Namanyele wanazaliwa kwa hiyo tukipoteza watu mia moja
au mia mbili Mh. Spika hakuna kitu kitakachopotea katika nchi hii,
tumeonewa vya kutosha haiwezekani" alisisitiza Ally Kessy na kuongeza;
"Mnasema
mnarekebisha mikataba, mikataba kurekebisha ni kutafuta hao wote
waliosaini wakamatwe, wanyang'anywe mali zao, wanyongwe tutabaki salama
katika hii nchi, itakuwa mfano, nataka comment ya serikali kusikia kuwa
tutashughulikia wote waliotia saini mikataba ya madini 1998 wakamatwe
mara moja" alisema Kessy
0 comments:
Chapisha Maoni