Aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.
Wilbroad Slaa amesema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha Mzee Philemon
Ndesamburo na kueleza jinsi walivyokijenga chama pamoja.
Dk.
Slaa amesema kuwa licha ya Ndesamburo kuwa na utajiri mkubwa, lakini
hakuuona kuwa ni kitu bali ni nyenzo ya kuwakomboa wananchi katika sekta
mbalimbali.
Dk.
Slaa ameitoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tangu aliyekuwa Mbunge wa
Moshi Mjini kwa miaka 15, Mzee Philemon Ndesamburo alipozikwa nyumbani
kwake KDC Moshi baada ya kufariki wiki iliyopita alivyopata matatizo
ghafla akiwa ofisini kwake.
Dk.
Slaa ambaye sasa anaishi Toroto nchini Canada baada ya kujiuzulu
wadhifa wake na kuachana na siasa tangu mwaka juzi, alisema kuwa
ameshtushwa sana na kifo cha ghafla cha kiongozi huyo tegemeo. Alieleza
kuwa licha ya wao kubaki na majonzi, lakini anaamini kazi ya Mungu haina
makosa wala haihojiwa.
"Ni
kweli nimefanya kazi na Ndesamburo, tumejenga CHADEMA kwa pamoja hasa
kipindi cha mwaka 2003 hadi 2005 ambapo tulizunguka nchi nzima," alisema
Dk. Slaa na kuongeza kuwa licha ya mazingira magumu waliyokutana naye
kwenye harakati za kukitangaza chama hicho, Mzee Ndesamburo hakulalamika
alipotakiwa kulala chini, lakini aliona hizo ni changamoto za kutafuta
ukombozi.
Aidha,
Dk. Slaa alisema kuwa Mzee Ndesamburo alikuwa msikivu na mwenye kuelewa
na kuwa tayari kuwasaidia wengi kwa hali na mali kwani mara kadhaa
alitoa mali zake kuwasaidia wagombea wa CHADEMA na hata yeye mwenyewe
kwenda kuwapigia kampeni bila kujali umbali aliotakiwa kwenda.
Akizungumzia
kifo chake, Dk. Slaa alisema kuwa kifo hicho ni cha kusikitisha kwa
sababu alifariki ghafla, hakupata nafasi ya kuagana na ndugu jamaa na
marafiki.
"Wakati
mwingine afadhai mtu akiugua mnajiandaa kisaikolojia, ila akifariki
ghafla tu, huwa ni kazi ngumu kuipokea ile hali.Kazi kubwa iliyobaki kwa
watanzania sasa ni kutekeleza yale yote ambayo Mzee Ndesamburo
amewaachia huku tukimuombea Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi."
Dk.
Slaa aliondoka nchini mwaka 2015 baada ya kujiuzulu wadhifa wake
kufuatia chama chake kumpokea na kumpa nafasi ya kugombea urais,
aliyekuwa kada nguli wa CCM, Edward Lowassa.
0 comments:
Chapisha Maoni