Na Veronica Martine, Sengerema
Mlinzi
mmoja wa maduka ameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na mwingine
mmoja kujeruhiwa katika kitongoji cha Sima Majengo Kata ya Sima
Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti
wa kitongoji hicho Martine Faustine amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kutaja jina la mtu aliyepoteza maisha kuwa ni Selemani Buyoga
(24) mkazi wa kitongoji cha Sima Majengo na aliyejeruhiwa ni Charles
Guli (55) mkazi wa Ngara mkoani Kagera wote wakiwa ni walizi wa
kampuni ya ulinzi inayofahamika kwa jina Nyuki ya Kahama Mkoani
Shinyanga.
“Mimi
taarifa hizo nimezipata saa 11 alfajiri baada ya mama mmoja kuja kwangu
na kunieleza nilifika eneo la tukio bila kukawia nikakuta watu wawili
mmoja akiwa ameferiki na mwingine amejeruhiwa,” alisema mwenyekiti wa kitongoji cha Sima Majengo.
Nae
Mwenyekiti wa kijiji cha Sima, Bahati Petro Mhangwa amewatupia lawama
wananchi kwa madai ya kushindwa kutoa taarifa kwa viongozi husika pale
wanapopata wageni katika maeneo yao na kuwahifadhi kwa siri na
kuwataka waachane na tabia hiyo mara moja.
“Ndungu
wanasima kiukweli hii hali inatisha mimi nilitegemea kwamba kwa sasa
Sima yetu tupo na amani kumbe sio hivyo jamani nawaombeni tushirikiane
kwa pamoja kuwafichua wanafanya vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na
kuwaleta wageni kwangu ili niwatambue naamini wageni hawa wanaokuja hapa
Sima bila taarifa ndiyo wanaosababisha matukio kama haya kutokea,” alisema Mwenyekiti wa kijiji cha Sima.
Diwani wa kata hiyo Makoye Sengerema Lugata amewataka wananchi kujenga desturi ya kutoa taarifa pindi matukio yanapotokea .
“Tukio
lilitokea saa saba usiku hadi saa moja wananchi hamjatoa taarifa kwa
viongozi kwa nini na nyinyi viongozi fanyeni hima kufuatilia matukio
kama haya wananchi wanatambua pengine hamtoi ushirikiano kwao niwasii
wananchi tushirikiane kwa pamoja kuwafichua walitekeleza mauaji haya,” alisema Diwani wa kata ya Sima.
Kwa
upande wao baadhi ya ndugu wa marehemu na wakazi wa kata hiyo
wamesikitishwa na tukio hilo, huku wakiiomba serikali kuimalisha ulinzi
katika kata hiyo ili kunusuru mauaji ya mara kwa mara .
“Mimi
nasema viongozi wetu hawako makini na kazi yao kwa sababu sisi
tunapojitahidi kuwapigia simu kiongozi anakwambia yupo Sengerema kwa
namna hii sioni kama tutafika mbali matukio yataendelea kutokea kwa
sababu hata ulinzi hapa haujaimarishwa,”walisema Ndugu wa Marehemu.
Jeshi
la Polisi limefika katika eneo la tukio na kuuchua mwili wa marehemu na
kuupeleka katika Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema kwenye chumba
cha kuhifadhia maiti huku mwingine aliyejeruhiwa akiendelea kupatiwa
matibabu.
Kufuatia
mauaji haya ya walinzi, kituo hiki kimemtafuta Mwenyekiti wa kamati ya
Ulinzi na Usalama ambae pia ni Mkuu wawila ya ya Sengerema, Emmanuel
Kipole ambapo ameyataka makumpuni yote ya ulinzi Wilayani Sengerema
yahakikishe yanaajiri walinzi wenye sifa stahiki waliopitia mafunzo ya
ulinzi.
“Hakuna
anayefurahishwa na matukio haya nitoe rai kwa makampuni yote ya ulinzi
wilayani Sengerema yahakikishe yanawakiki walinzi wao kama wanasifa za
kuwa walinzi kama hawana waache kazi,” alisema Mkuu wa wilaya.
Matukio
ya walinzi kuuawa yameendelea kushika kasi katika Wilaya ya Sengerema
Mkoani Mwanza ambapo mbali na matukio hayo ya walinzi kutokea katika
kata hiyo mapema mwaka jana watu saba wa familia moja walipoteza maisha
kwa kukatwa katwa na mapanga na watu wasiofahamika huku chanzo chake
kikiwa hakifahamiki.
0 comments:
Chapisha Maoni