Hatimaye
Kenya imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuanza kutumia vidonge vya
ugonjwa wa Ukimwi ambavyo vinaweza kuboresha afya na kurefusha maisha ya
maelfu ya watu wanaosumbuliwa na magonjwa nyemelezi na ambayo
hayakubali tiba nyingine.
Jina
la dawa hiyo kitaalamu ni Dolutegravir (DTG), lakini itajulikana kama
Tivicay, na inazalishwa na ViiV Healthcare, kampuni ambayo sehemu kubwa
ya hisa zake inamilikiwa na GlaxoSmithKline.
DTG
imekuwa dawa ambayo ni chaguo la kwanza la watu wanaoishi na Virusi vya
Ukimwi (VVU) kwa miaka miwili iliyopita katika nchi za watu wenye
kipato kikubwa kwa kuwa ina athari chache, ni rahisi kutumia kuliko dawa
za ARV zinazotumika sasa (yaani kidonge kimoja kidogo kila siku).
Kwa kutumia dawa hiyo, kuna uwezekano mdogo kwa wagonjwa kutengeneza usugu, kwa mujibu wa tovuti ya unitaid.eu.
Mwaka
2015, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilipendekeza DTG iwe chaguo la
kwanza kwa watu wazima na vijana, lakini hadi siku za karibuni watu
wanaoishi na VVU katika nchi kama Kenya walikuwa hawawezi kupata dawa
hizo.
Vidonge
hivyo, ambavyo vilipitishwa kutumika nchini Marekani mwaka 2013, sasa
vinagawiwa kwa wagonjwa 20,000 nchini Kenya kabla ya kupelekwa Nigeria
na baadaye Uganda, kwa kusaidiwa na Unitaid, ambao ni wakala wa afya.
DTG ni dawa ambayo inatumiwa na watu wenye VVU ambao hawakuwahi kutumia dawa za kufubaza makali ya Ukimwi ya ARV.
“Nilikuwa
na tatizo la mara kwa mara la kutokuwa na hamu ya kula,” alisema mkazi
wa Nairobi, Doughtiest Ogutu alipozungumza na taasisi ya Reuters
Foundation.
Ogutu alianza kutumia dawa hizo mwaka huu kwa sababu tiba nyingine hazikuwa zinamfaa.
“Hamu yangu ya kula imerejea, mwili wangu unafanya kazi vizuri.”
Ogutu,
ambaye ameishi na VVU kwa miaka 15, alisema kiwango cha VVU mwilini
mwake kimepungua kwa kiasi kikubwa kutoka virusi 450,000 hadi 40,000
tangu aanze kutumia DTG.
Nchi
za kusini mwa Jangwa la Sahara zimekuwa zikiathiriwa sana na Virusi vya
Ukimwi kwa miongo kadhaa na karibu robo tatu ya wakazi wake wana Virusi
vya Ukimwi na Ukimwi.
Shirika
la Umoja wa Mataifa la Ukimwi (UNAIDS) linalenga kuwa asilimia 90 ya
watu watakaogundulika kuwa na VVU wawe wamepata dawa hiyo ifikapo mwaka
2020.
Karibu
asilimia 15 ya wagonjwa wa VVU hawawezi kutibiwa kwa kuwa dawa
hazifanyi kazi mwilini mwao, alisema Sylvia Ojoo, mkurugenzi wa Shule ya
Afya ya Chuo Kikuu cha Maryland nchini Kenya, ambaye anasimamia dawa
hizo.
0 comments:
Chapisha Maoni