test

Jumanne, 6 Juni 2017

Ally Kessy: Wabunge Wanaotusumbua Bungeni Wapimwe Madawa ya Kulevya


Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amependekeza kuwapo na sheria ya kuwapima wabunge matumizi ya dawa za kulevya ili kuepukana na ukorofi unaojitokeza bungeni mara kwa mara.

Keissy alisema hayo jana bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa mstari wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule atakayebisha kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge.

"Tutengeneze sheria sisi sote hapa tupimwe, inawezekana kuna watu wanatumia madawa ya kulevya humu, tena mimi nitakuwa wa kwanza, tupimwe kuondoa tatizo kwenye bunge letu hili la ukorofi na atakayekataa apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge haiwezekani kurudia makosa mtu mmoja kila siku anasemwa anarudia yale yale"  alisema Keissy na kuongeza;

"Adhabu ndogo hii lazima ziwe kali wasipate chochote, wasionekane bungeni muda wa miezi sita au saba ndiyo watashika nidhamu katika bunge hili. Haiwezekani tunaonekana kama tupo Manzese, wabunge wa mjini wamezoea kwenye vijiwe sisi wabunge wa bara hatutaki mchezo mchezo namna hii ya kutukana. Spika kwanza anawazidi umri pamoja na cheo"

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni