Na Regina Mkonde
Viongozi
wa vyama vya siasa vya upinzani wamelaani kitendo cha serikali ya mkoa
wa Kilimanjaro cha kuzuia uwanja wa Mashujaa kutumika kwa ajili ya ibada
ya kuaga mwili wa marehemu Philemon Ndesamburo, na kudai kuwa kililenga
kuendeleza chuki ya kisiasa.
Katika
hatua nyingine, wameshangazwa na CCM kutokuwa na muwakilishi katika
ibada ya kuuga mwili wa Ndesamburo aliyefariki dunia wiki iliyopita
wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alisema kitendo hicho kimelenga kudhibiti demokrasia. “Nawapongeza
kwa maandalizi haya. ila kwa hili inaonyesha jitihada za kudhibiti
demokrasia zinaendelea, watu hawa ni wa kuwasamehe bure."
Naye mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Pwani, Fredrick Sumaye alisema “Hata
njia za kupitisha maiti nazo zinalindwa hizi chuki tukiacha zijengwe
hatutakua hai, wananchi hatutaweza kuwaonea muda mrefu. Ila mbegu ya
amani aliyoipanda Ndesamburo itaendelea kuzaa aliyoyasimamia.”
Wakati
akitoa salamu hizo, Mwenyekiti mwenza wa UKAWA, James Mbatia alisema
kitendo cha viongozi wa CCM kutohudhuria kwenye ibada hiyo si cha
kiungwana kwani kinalenga kugawa wananchi kwa misingi ya vyama.
“Walichofanya
leo sio cha kiungwana, watanzania tusikubali kugawanyishwa kwa misingi
ya imani wala vyama, sijauona uwakilishi wa CCM, tuwasamehe na mimi
nimewakilisha CCM wote hapa ili tulete amani ya mzee Ndesa.Ndesamburo
alikuwa analeta watu wote pamoja, lakini leo hata njia za kupitisha
mwili wake nazo zinalindwa hizi chuki tukiacha zijengwe hatutakua hai,” alisema.
Kwa
upande wa Makamu Mwenyekiti CUF Severina Mwijage wakati akitoa salamu
za rambirambi alisema amesikitishwa na kitendo cha kuzuiwa uwanja kwani
marehemu Ndesamburo alishiriki kuujenga uwanja huo.
“Siasa
za sasa hivi ni hatari, za kupandikiza watu chuki ni mbaya sana, na
mimi naomba niongezeee wenyewe wanajua chuki ndio chama chao
kitakachosaidia kuchukua dola, sisi tunachaguliwa na wananchi tunajua
matatizo ya wananchi, aelewe yule anayewachonganisha itakuaje yeye
ambaye aliyemchagua atakuja na kuondoka na yeye atabaki katika mkoa na
watoto wake wanaishi na wananchi,” alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni