Watumishi
zaidi ya sabini wamesimamishwa kazi wilayani Misungwi Mwanza kwa
kukutwa na vyeti feki, ubadhilifu wa mali za Umma na utovu wa nidhamu.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Misungwi Bw. Athon Masele amesema kuwa watumishi 68
wamekutwa na vyeti feki, wawili walikuwa ni wabadhilifu wa mali za Umma
huku wengine wawili walikuwa ni watovu wa nidhamu, jambo ambali
limepelekea idara ya elimu na afya kuathirika kwa kiwango kikubwa zaidi.
Kwa
upande wake Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mh. Charles Kitwanga amesema
mwaka jana walisimamishwa kazi watumishi wawili kwa tuhuma za ubadhilifu
wa mali za umma ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja mapato
yameongezeka kwa kiwango kikubwa kutoka kiasi cha shilingi milioni 24
hadi shilingi milioni 120 kwa mwezi hali iliyosaidia kupata hati safi
baada ya CAG kuridhishwa na utendaji kazi wa halmashauri
0 comments:
Chapisha Maoni