WANAFUNZI
wanaokwenda kusoma vyuo vikuu vya nje wanatakiwa kupita katika Tume ya
Vyuo Vikuu nchini (TCU) kwa ajili ya kuangalia vigezo ambavyo
vinahitajika.
Hayo
yamesemwa na Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk.
Fabian Mahundu wakati wa maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India
yaliyofanyika katika ubalozi wa nchi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Dk.
Mahundu amesema mwanafunzi anayekwenda kusoma vyuo vya nje anatakiwa
kuwa na ufaulu wa D mbili ambazo ni viwango vilivyowekwa.
Amesema
kuwa mwanafunzi anayekwenda kusoma nje bila kupita katika tume hiyo
ilivyowekwa kwa ajili ya kuratibu, akirudi anakuwa anakosa sifa katika
mfumo wa elimu nchini.
Kwa
upande wa Balozi wa India nchini, Sandeep Arya amesema kuwa Tanzania
na India zimekuwa na mahusiano mazuri katika nyanja mbalimbali. Amesema
India imekuwa ikitoa elimu bora na kwamba Tanzania ni nchi ambayo
inanufaika kwa kupata ufadhili wa watu 25 kila mwaka.
Naye,
Mkurugenzi wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel amesema
kuwa nchi ya India iangalie uwezekano wa kuongeza idadi ya ufadhili
hadi kufikia 100 kutokana na mahitaji yaliyopo.
Amesema kuwa GEL imekuwa katika msisitizo wa mara zote katika kuhakikisha wanafunzi wote wanapita TCU kwa ajili ya kuhakikiwa..
Maonesho vya vyuo vikuu vya nchini India yamefadhiliwa a kampuni ya Global Education Link (GEL).
Afisa
Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Dk.Fabian
Mahundu akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India
vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa India Nchini Tanzania, Sandeep Arya akizungumza akizungumza katika
maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozini
Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel
akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India
vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Udahili wa Global Education Link (GEL), Zakia Nassor akitoa elimu
kwa wanafunzi waliotembelea banda katika maonesho ya vyuo Vikuu vya
nchini India vilivyofanyika katika Ubalozini Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Afisa
Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk.Fabian Mahundu
akiwa na Balozi wa India nchini, Sandeep Arya pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel
wakitembelea mabanda katika maonesho ya vyuo vikuu vya nchini
India.leo jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa India nchini, Sandeep Arya akiwa katika picha ya watanzania 25
waliopata ufadhili wa Serikali ya India wa kusoma katika vyuo vikuu vya
nchi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni