Simba
imetwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwa kuifunga Mbao kwa mabao 2-1
kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na kufuzu kucheza Kombe la Shirikisho
Afrika mwakani.
Simba
ilipata mabao yake mawili yaliyofungwa na washambuliaji wake Fredrick
Blagnon na penalti ya Shiza Kichuya wakati bao la kufutia machozi kwa
Mbao lilifungwa na Ndaki Robert.
Katika
mchezo huo wa fainali timu zote mbili zilicheza kwa nguvu na kujilinda
kwa umakini hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika timu hizo zilikuwa
suruhu.
Kipindi
cha pili kila timu ilifanya mabadiliko lakini uamuzi wa Joseph Omog
kumtoa Said Ndemla dakika 83 na kuingia Fredrick Blagnon uliokuwa ni
habari njema kwa Simba.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alifungia Simba bao la kwanza katika
dakika 95, lakini Mbao ilisawazisha dakika 109 kupitia Ndaki.
Wakati
mashabiki wakiamini mechi hiyo itakwenda kwenye penalti katika dakika
116, uamuzi wa utata wa mwamuzi Mohamed Kikumbo ulifaidisha Simba kwa
kupata penalti.
Uamuzi
ulisababisha wachezaji wa Mbao kumvaa mwamuzi Kikumbo wakipinga uamuzi
huo na kusababisha askari kuingia uwanjani kutuliza ghasia.
Baada
ya vurugu hizo mpira uliendelea kwa Kichuya kupiga penalti hiyo na
kuifungia Simba bao la pili na ushindi na kuamsha shangwe uwanjani hapo.
A
wali
milango ya Uwanja wa Jamhuri ulifungwa saa 8.00 mchana baada ya
majukwaa yote kujaa. Ukikadiriwa kutimiza idadi ya mashabiki 23,000
idadi iliyotangazwa na shirikisho la soka Tanzania (TFF) na chama cha
soka Dodoma (Dorefa)
Kitendo
cha timu ya Simba kutoonekana wakishuka kwenye basi uwanjani
kimeonekana kuwashangaza mashabiki wengi waliofika kutazama pambano hili
la fainali.
Mchezo huo unaochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma umevuta hisia nyingi za mashabiki waliofurika na kujaza uwanja huu.
Lakini
katika hali isiyotarajiwa na wengi basi la timu ya Simba SC lililoingia
uwanjani lilikua tupu na waliokua ndani yake ni wachezaji wanne pekee.
Baada ya basi hilo kuingia ndani baadhi ya mashabiki walibaki kujiuliza walipo wachezaji hao.
Wachezaji
wa Simba kabla ya kuanza mpira wote waliinama na kufunga viatu vyao
wakati wa Mbao walienda kupiga magoti kwenye lango lao
Simba ilianzisha mpira kwa kuupiga nje jambo ambao ni kushangaza katika soka.Simba
ilianza mechi kwa kasi na dakika ya 10, Laudit Mavugo anapiga shuti
linalopaa akishindwa kumalizia mpira uliookolewa vibaya na mabeki wa
Mbao
Mbao
ilijibu mapigo kupitia Pius Buswita nusura aipatie bao akishindwa
kumalizia mpira uliotemwa na kipa Daniel Agyei wa Simba kutokana na
faulo ambayo ilipigwa na Jamal Mwambeleko
Dakika ya 34, Mavugo anapiga shuti linalombabatiza Yussuf Ndikumana na kuwa kona ambayo haijazaa matunda.
Jamal Mwambeleko wa Mbao anapewa kadi ya njano dakika ya 43 kwa kumchezea rafu Mohammed Hussein 'Tshabalala'Kabla
ya kipindi cha pili kuanza, mmoja wa wachezaji wa Mbao alienda kumwagia
maji milingoti ya lango lake ikiashiria kama imani za kishirikina.
Dakika ya 54 mshambuliaji wa Mbao, Habib Hajji anakosa bao la wazi kwa kupiga nje.
Mbao wanafanya mabadiliko anatolewa George Sangija na kuingia Dickson Ambundo wakati
Simba inamtoa Juma Luizio na kuingia Ibrahimu Ajib
Dakika ya 51, Simba wanamtoa Mohammed Hussein na kumuingiza Abdi Banda, dakika 83, Simba inamtoa Ndemla anaingia Blagnon.
0 comments:
Chapisha Maoni