Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amefunguka kuwa
wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala wameiba jumla ya kete 32 za dawa za
kulevya zilizokuwa kwenye mwili wa Raia wa Ghana aliyefariki dunia
akiwa katika nyumba ya wageni.
Kamanda
Sirro amesema wahudumu hao wanne wote wamekamatwa na kukiri kwamba
baada ya kifo cha raia huyo wa Ghana aliyefariki ndani ya 'Red Carpet'
iliyopo Sinza Dar es Salaam walipasua mwili wa raia huyo na kutoa kete
hizo kisha kuziuza, na kuongeza wametaja watu ambao wamewauzia ambao nao
wamekamatwa na wapo chini ya ulinzi wa polisi
"Yule
Mghana ambaye alikutwa amefariki dunia tarehe 14/ 03/ 2017 kwenye
nyumba ya wageni ya 'Red Carpet' na alichukuliwa na kupelekwa mochwari
Mwananyamala lakini inaonekana wale wahudumu wali[pata taarifa kuwa ule
mwili una dawa za kulevya, kimsingi walikula njama wakampasua na kutoa
kete 32 za madawa ya kulevya na baada ya kuyapata waliyauza hayo madawa"
alisema Sirro
Kamanda Sirro aliendelea kusema kuwa mpaka sasa wanawashikilia watu wanne ambayo wamehusika katika jambo hilo.
"Mpaka
sasa tunawashikilia watu wanne ambao wanakiri kupasua mwili huo ambao
ni wahusika wakuu na ni wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala lakini
tumekwenda mbali zaidi baada ya kufanya upasuaji wamemuuzia nani naye
amekatwa pia na anaeleza kuwa alinunua hayo madawa, lakini pia naye
alichukua na kumuuzia mtu mwingine anayefahamika kwa jina la Ally
Nyundo, huyu Nyundo tulishamkataga na kumpeleka kwa Mkemia Mkuu yeye
alionekana ni mtumiaji, kimsingi tuna hao watuhumiwa wanne na huyo wa
tano aliyekamatwa sasa tunaandaa jalada" alisisitiza Sirro
0 comments:
Chapisha Maoni