Picha
ya pamoja ya wadau wa elimu Tanzania na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya
Bunge, huduma na Maendeleo ya Jamii baada ya kikao cha kuwasilisha
mapendekezo ya wadau wa elimu katika bajeti ya elimu ya mwaka wa fedha
2017/2018 uliofanyika katika ukumbi mdogo wa bunge mjini Dodoma.
Baada
ya Kikao hicho wanakamati ya bunge ya kudumu huduma na maendeleo ya
jamii waliahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na wadau wa
elimu ili kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini Tanzania.
Makamu
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kudumu huduma na maendeleo ya jamii,
Mhe. Azzan Zungu akifungua kikao na kuwakaribisha wadau wa elimu
waliofika katika mkutano huo ili kuwasilisha mapendekezo na maoni kuhusu
bajeti ya elimu ya mwaka 2017/18.
Kiongozi
wa wadau wa elimu Tanzania(Head of Deligation) , Ndugu Saddam Khalfan
akielezea madhumini ya kikao hicho kilichokuwa kinahusiha kuwasilisha
mapendekezo na maoniya wadau wa elimu katika bajeti ya elimu ya mwaka
2017/18 kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa Bunge mjini Dodoma.
Mwakilishi
wa Mtandao wa Elimu Tanzania, Ndugu Karoli Kadeghe kutoka ACTIONAID
Tanzania akiwasilisha mapendekezo ya wadau wa elimu kuhusu serikali
kuongeza uwekezaji wa fedha za ugharamiaji elimu kupitia rasilimali za
ndani ili kuepukana na utegemezi wa fedha za wahisani kwa wajumbe wa
kamati ya Kudumu ya Bunge huduma na maendeleo ya jamii kwenye mkutano
uliofanyika katika ukumbi mdogo wa Bunge mjini Dodoma.
Pia
aligusia umuhimu wa uwekezaji wa miundombinu ya shule na kuboresha
maslahi ya walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi.
Katibu
mtendaji wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania, Ndugu Alphonce Lusako
akihimiza na kuishauri kamati ya bunge kuisimamia serikali kutoa bajeti
ya kutosha kwa ajili ya wanafunzi wote wenye sifa wanaodahiliwa vyuo
vikuu nchini bila ubaguzi wowote. Bajeti husika ijikite katika maboresho
ya mafunzo kwa vitendo kazi (Internship), mafunzo ya ufundi stadi na
kuongeza bajeti ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Pia
aliiomba kamati hiyo kutoa pendekezo kwa Serikali kupitia Bodi ya Mikopo
kuweka utaratibu thabiti na endelevu wa Kukusanya fedha za mikopo kwa
wanufaika waliokwisha nufaika na mikopo hiyo ilikuongeza Wigo wa kuwapa
mikopo wanafunzi wapya wa vyuo vikuu nchini.
Pia
tunaiomba serekali Ilitazame upya suala la ukusanyaji wa madeni ya
walionufaika na mikopo, kubadilisha ghafla Makusanyo toka asilimia nane
(8%) hadi asilimia kumi na tano(15%) ni kuvunja mkataba wa mkopaji na
mkopeshaji, jambo hili linavunja sharia. Kama ni lazima kufanya hivyo
basi makusanyo hayo ya asilimia kumi na tano (15%) yaanzie kwa hawa
wanaokopeshwa sasa ili wakope wakiwa wanalijua hilo.
Baadhi
ya wanachama wa Mtandao wa elimu Tanzania(Ten Met) wakichangia mada
kuhusu bajeti ya elimu katika masuala kama kuruhusu wanafunzi waliopata
ujauzito kurudi mashuleni, upungufu wa madarasa pamoja na vitendea kazi
vya elimu.
Wajumbe
wakiangalia video ya hali halisi ya baadhi ya shule nchini pamoja na
makazi ya walimu iliyoandaliwa na ActionAid Tanzania na Ten Met.
0 comments:
Chapisha Maoni