Mkuu
wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Nyakoro Sirro amesema kuwa lengo lake
kubwa baada ya kukabidhiwa wadhifa huo mpya ni kuhakikisha kuwa uhalifu
unapungua na anaimani kubwa kuwa atafanikiwa kwa sababu wananchi ambao
ni wema ni wengi kuliko ambao ni majambazi.
Simon
Sirro ameyasema hayo leo mara tu baada ya kupandishwa cheo na kuwa
Inspeka Jenerali wa Jeshi la Polisi na kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la
Polisi akichukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Aidha,
IGP Sirro amewaomba wananchi kutoa ushirikiano ili wafanikiwe
kutokomeza uhalifu kwa sababu wahalifu wanaishi ndani ya jamii, hivyo
Polisi peke yao hawatafanikiwa.
“Ombi
langu kwa Watanzania, ili tuweze kuishi kwa amani na utulivu, ni vizuri
sana wakatoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi. Naamini kabisa tutaweza
kwa sababu hawa wahalifu ni wachache na sisi ni wengi, kwa hiyo umoja
wetu ule ni lazima tutashinda” amesema IGP Sirro wakati akihojiwa na maafisa wa habari wa Ikulu.
Mbali
na kuomba ushirikiano huo kwa raia, IGP Sirro ametoa onyo kwa wahalifu
kuwa, siku zote uhalifu haulipi, na ukiung’ang’ania sana, utasababisha
ukaiacha familia yako.
Msikilize hapa chini IGP Sirro akizungumza;
0 comments:
Chapisha Maoni