Serikali
iko kwenye mpango wa kuongeza ndege nyingine moja ili zizidi kufika
sehemu nyingi zaidi Tanzania ambapo Naibu Waziri wa wizara ya Ujenzi,
uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amesema July 2017 ndio
inanunuliwa nyingine.
Amesema
Ndege hiyo itakayonunuliwa July ni aina ya Dash 8-Q 400 ambapo hatua
hiyo italifanya shirika la ATCL kufikisha Ndege nne (4) ambazo
zitaongeza safari zake kwa kuhudumia masoko yake ya ndani na miji ya
Nchi jirani kama vile Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi, Zambia na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).
Ni
kauli ambayo aliitoa wakati wa uzinduzi wa safari za Ndege za ATCL
kwenye mkoa Tabora na kuongezea kwamba lengo la Serikali ni kuhakikisha
hadi kufikia July 2018 Shirika la Ndege Tanzania liwe linamiliki Ndege
sita zenye uwezo wa kubeba abiria kwa kiwango tofauti tofauti na
kusafiri mikoa mingi na nje ya Tanzania.
Naibu
Waziri alisema hadi sasa Serikali imeshanunua ndege mbili aina ya
Bombardier Dash 8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na
hatua inayofuata ni ununuzi wa ndege nyingine tatu aina ya Bombardier
Dash 8-Q400 yenye uwezo kubeba abiria 76, CS 300 mbili zitakazobeba
abiria 132 kila moja na Boeing 787 ya kubeba abiria 262.
Alisema
kuwa hatua hiyo inaenda sambamba na uimarishaji wa Shirika la Ndege
hapa nchini na ujenzi wa viwanja vipya vya ndege katika mikoa ambayo
haina viwanja hivyo kwa sasa ili ifike siku mikoa yote Tanzania iweze
kuunganishwa na usafiri wa anga