Mzozo
mpya umeibuka kati ya tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, na vinara wa
mrengo wa upinzani wa NASA kuhusu utangazaji wa matokeo rasmi ya kura za
Urais.
Tume
Huru ya Uchaguzi na Mipaka ‘IEBC’ imeijibu mrengo wa upinzani wa NASA
kufuatia vitisho vyake vya kususia uchaguzi iwapo tume hiyo itafaulu
kwenye rufaa iliyowasilisha mahakamani dhidi ya uamuzi wa mahakama
ulioruhusu matokeo ya kura za Urais kutangazwa katika kituo cha kupigia
kura.
Hii
ni baada ya viongozi wa upinzani kuishauri IEBC dhidi ya kusaka njia za
kubadili mipango hiyo ili kutangaza matokeo ya kura za Urais katika
kituo cha kitaifa jinsi ilivyokuwa matokeo ya miaka iliyopita.
Tume
hiyo kupita mwenyekiti wake Wafula Chebukati, imeeleza kuwa haitobadili
msimamo wake wa kukata rufaa na kuwaambia viongozi wa upinzani
kuheshimu mahakama na kutumia njia za kisheria kutatua malalamiko yao.
Viongozi
wa mrengo wa upinzani wakiongozwa na Mgombea wa Urais, Raila Odinga,
walitishia kususia uchaguzi iwapo tume hiyo itakata rufaa na kuruhusu
matokeo ya Urais kutoka kila kituo kutangazwa kitaifa.
Taifa
la Kenya linatarajiwa kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais baadaye mwaka huu
huku ushindani mkali ukitarajiwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta anayewania
kiti hicho kupitia mrengo wake wa Jubilee na Raila Odinga, anayebeba
bendera ya mrengo wa Upinzani wa NASA.
0 comments:
Chapisha Maoni