.
Rais
wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameitaka Uganda kubadili jina la Ziwa
Victoria ili liendane na jina linalowakilisha uhalisia wa wananchi wa
eneo hilo.
Kiongozi
huyo anayekosolewa vikali nchini mwake amesema tayari amemfahamisha
Rais Yoweri Museveni juu ya haja ya kubadilishwa jina hilo.
Jina
la Ziwa Victoria lilitolewa na mtafiti mmoja wa Uingereza kama zawadi
kwa Malkia wa Taifa hilo aliyetambulika kwa jina la Victoria.
Akizungumza
katika ufunguzi wa maonyesho ya utalii mjini Kampala, Rais Zuma amesema
Ziwa hilo kuendelea kuitwa Victoria kunawanyima fursa wananchi wa
eneo hilo kujivunia uasili wao.
“Mnaweza
kuweka bango kubwa linaloonyesha jina la jipya na kisha mkaweka bango
dogo litakalosomeka kama “ zamani eneo hili liliitwa Ziwa Victoria”.
Lazima mbadilishe jina hili na kuweka jina litakaloelezea uzuri wa Taifa
hili,” amesema Rais Zuma.
0 comments:
Chapisha Maoni