test

Jumatano, 31 Mei 2017

Mwili wa mwanahabari Rweyemamu kuzikwa Kagera


Responsive image
Marehemu Chrysostom Rweyemamu.

Mwili wa mwanahabari nguli nchini Chrysostom Rweyemamu aliyefariki dunia  Jumamosi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam umeagwa leo kwa kusafirishwa kwenda Muleba Mkoani Kagera kwa mazishi.

Mwili wa Marehemu Rweyemamu umeagwa Mbweni katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu RAPHAEL na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri - TEF, Theophil Makunga na mwanahabari Dokta Gideon Shoo wamemwelezea Marehemu Rweyemamu kuwa mtu aliyekuwa mahiri katika tasnia ya habari aliyekuwa na mchango mkubwa katika hifadhi ya mazingira.

Marehemu Rweyemamu pia anakumbukwa kama mwalimu wa taaluma ya habari.

Katika uhai wake Chrysostom Rweyemamu amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika tasnia ya habari ikiwemo kufundisha katika Chuo Cha Uandishi wa Habari - TSJ.

Bwana Ametoa Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni