Jeshi
la Polisi mkoani Tanga jana lilifunga barabara ya kutokea Dar es
salaam kuelekea Arusha kufuatia eneo la Mombo mkoani Tanga kuangukiwa na
maporomoko ya mawe pamoja na matope na kusababisha athari kwa baadhi ya
magari
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani humo Benedict Wakuyamba alisema, maporomoko hayo yalisababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani humo na maeneo mbalimbali nchini
"Hali
ya mvua imeendelea kunyesha na kufukia barabara eneo la Mombo kutokea
Dar es salaam kuelekea Arusha ambapo matope na miti vimesombwa na
kukwama barabarani hali iliyokwamisha magari makubwa kwa madogo kusafiri
kupitia eneo hilo..
"Niwaombe
abiria au wananchi kwa ujumla kama hawana ulazima wa kusafiri kwenda
mikoa ya Kaskazini ni vizuri wakatulia kwa siku mbili tuone hali
inakwendaje kwa ajili ya usalama wao". Alisema Kamishna Msaidizi Benedict
Kwa
upande mwingine Kamishna huyo alisema TANROADS na Jeshi la Polisi
mkoani humo wanaendelea kusaidia kuondoa magogo na tope zilizosakama
katika barabara ili kunusuru hali ya usafiri.