Aliyekuwa
Naibu Waziri wa Fedha katika Serikali ya Awamu ya Tatu, na Mbunge wa
Mkuranga, Adam Kighoma Ali Malima amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo akituhumiwa kumzuia Polisi
kutekeleza majukumu yake.
Malima
anatuhumiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2017 eneo la Masaki karibu na
Ubalozi wa Canada jijini Dar es Salaam jana majira ya saa sita mchana,
ambapo Polisi walikuta ameegesha gari lake sehemu isiyotakuwa na
alipotakiwa kulipeleka ‘yard’ alikataa.
Polisi
hao walikuwa wameambatana na maofisa wa kampuni moja ambayo ni wakala
wa kukusanya madeni, kukamata teksi bubu pamoja na kukamata magari
ambayo yanaegeshwa sehemu ambayo si sahihi kisheria.
Licha
ya Malima kuelezwa ukweli kuwa hakuwa ameegesha gari sehemu sahihi,
lakini alikataa kulipeleka alikoambiwa jambo lililoibua mtafaruku
mkubwa.
Baada ya kufikishwa mahakani yeye na dereva wake, wameachiwa kwa dhamana ya TZS milioni 5.
0 comments:
Chapisha Maoni