Akizungumza na Mwananchi leo, Lema amesema Ndesamburo alifika ofisini kwake asubuhi kama ilivyo kawaida yake lakini aliugua ghafla mnamo saa nne asubuhi.
Bazil alisema baada ya Ndesamburo kujisikia vibaya, alichukuliwa na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC na wakati madaktari wanakifanya jitahada za kumpa matibabu alifariki dunia.
“Baada ya mwili kufanyiwa uchunguzi taarifa rasmi kuhusu kifo chake zitatolewa na uongozi wa chama pamoja na familia,” amesema
Wakati huo huo wanachama wa Chadema wamekusanyika kwa makundi katika eneo la hospitali wakionekana kuwa sura za huzuni.
0 comments:
Chapisha Maoni