test

Jumatano, 31 Mei 2017

Mwenge wa Uhuru leo umemaliza mbio zake katika Jiji la DSM


MWENGE DSM
Mwenge wa Uhuru leo umemaliza mbio zake katika Jiji la dsm baada ya kumaliza kuzindua miradi mitano katika manispaa mpya ya Ubungo iliyogharimu kiasi cha shilingi biilion mbili.

Miradi hiyo iliyozinduliwa ambayo baadhi yake imewekwa mawe ya msingi ni pamoja na ujenzi wa jengo jipya la kutolea huduma za watu wenye VVU lilipo mbezi ambalo litahudumia kata tano za wilaya ya Ubungo,kituo cha polisi cha daraja C kilichopo Kibamba Gogoni pamoja na ujenzi wa madarasa nane mapya ya shule ya msingi maramba mawili.

Miradi mingine ni pamoja na uzinduzi wa kituo cha mabasi cha simu 2000 Kilichopo sinza pamoja na zahanati katika eneo la mburahati.
Kiongozi wa mbio za mwenge Mwaka huu Amour Hamid Amour amewataka wananchi kuunga mkono serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea mamendeleo lakini pia kupambana na rushwa,ufisadi pamoja na kuenea kwa magonjwa yakiwemo malaria na VVU.

Wakizungumzia Uzinduzi wa miradi hiyo na faida yake kwa wananchi mganga mfawidhi wa zahanati ya mbezi pamoja na diwani wa eneo hilo wanaeleza.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni