Mmiliki
wa shule ya Lucky Vicent Arusha Innocent Moshi na Makamu Mkuu wa shule
Longino Vicent Nkana jana wamefikishwa Mahakamani na kusomewa makosa
matano.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali Rose Sule alisema mnamo May 6 Mmiliki huyo wa
shule aliruhusu Dereva kuendesha gari la abiria bila kuwa na leseni ya
usafirishaji, kutumia gari bila kuwa na BIMA pamoja na kushindwa kuingia
mkataba na Mwajiriwa.
Makosa
mengine ni kuzidisha abiria 13 kwenye gari pamoja kaimu mkuu wa chuo
kuratibu safari pamoja na kuruhusu gari kuzidisha abiria.
Watuhumiwa
wote waliachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuwa na watu wawili kwa bondi
ya milioni 15 kila mmoja na huku washtakiwa kutoruhusiwa kuondoka ndani
ya mkoa ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hati zao zakusafiria.
Hakimu
wa Mahakama ya hakimu mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Desdery
Kamugisha aliahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 8 mwezi wa 6 kutokana na
upelelezi kutokamilika.