Mrembo
wa Tanzania, Diana Edward amewataka warembo wanaoshiriki katika
mashindano ya Miss Tanzania kuwa wavumilivu ili kukabiliana na
changamoto mbalimbali za mashindano hayo zinazotokana na matatizo ya
kiuchumi.
Shindano
la Miss Tanzania lilifanyika Oktoba 29 mwaka jana mjini Mwanza na
kampuni ya Lino ilishindwa kukabidhi zawadi ya gari baada ya mdhamini
wa kwanza aliyeahidi kutoa zawadi hiyo kujitoa hatua za mwisho baada ya
shindano hilo kuhamia Mwanza.
Kutokana
na hali hiyo, kampuni ya Lino ilihaha kila kona kutafuta mdhamini
wengine na kuwapata uzalishaji na usambazaji wa vipodozi asilia, Grace
Product Ltd na duka la kuuza vito ya Gift Jewellers ambapo kwa pamoja
waliamua kununua gari aina ya Suzuki Swift yenye thamani ya Sh 9milioni
liyosajiliwa kwa namba T625DKL.
“Mbali
ya kuwa mvumilivu, mrembo unatakiwa kuwa na nidhamu, nilisubiri zawadi
hii kwa muda mrefu, najua matatizo ambayo yalikuwepo na ndiyo maana
nilivumilia mpaka hii leo (jana), nashukuru kwa kupata zawadi na sasa
nitaendelea vizuri na shughuli zangu za kazi za jamii,” alisema Diana.
“Naomba
warembo wajitokeza kushiriki katika mashindano ya urembo, ni
mashindano mazuri sana yenye kujenga mtu na kumpatia kipato, tokea
nimalize mashindano, nimeweza kupata dili mbalimbali ambazo sikutaka
kuziweka wazi kwenye jamii, zimekuwa ni shughuli zangu za kila siku,”
alisema.
Mkuu
wa Itifaki wa Kampuni ya Lino, Albert Makoye alisema kuwa wameishukuru
wadhamini wao na kwa sasa wanaanza pilika pilika za mashindano ya mwaka
huu.
“Ni
faraja, tulipewa muda wan a serikali kuwa ifikapo Mei 30 mwaka huu tuwe
tayari tumekamilisha zawadi za warembo, tumefanikisha kupata gari
kutoka kwa Grace Products na Gift Jewellers, sasa tunaanza ukurasa
mwingine,” alisema Makoye.
Mkurugenzi
wa Grace Products ltd, Elizabeth Kilili alisema kuwa ameamua kudhamini
zawadi ya gari kutokana na kuvutiwa na mashindano na hasa Diana ambaye
anatumia vipodozi vya asili.
Mhasibu
Mkuu wa duka la Gift Jewellers, Faudhia Salum alisema kuwa wamemua
kuwezesha zawadi ya gari hiyo, kama moja ya shughuli zao za kijamii.
Salum alisema kuwa wao kama wauzaji wa vito wamefarijika sana kusaidia
mashindano hayo na hasa ukizingatia kuwa vito vingi uvaliwa na akina
dada kwa lengo la kupendeza.