Katibu
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Bungu wilayani Kibiti, Alife
Mtulia ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani
kwake.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema mauaji hayo yamefanyika
usiku wa kuamkia leo (Jumapili) katika Kijiji cha Nyambunda.
Amesema
Mtulia aliuawa na watu hao alipokuwa anakwenda kuoga.Kamanda amesema
mwili wa marehemu umepelekwa kituo cha afya cha Kibiti kwa uchunguzi.
Mauaji
ya askari Polisi, viongozi wa Serikali za Mitaa na raia yamekuwa
yakifanyika mara kwa mara katika wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga
mkoani Pwani.
Jumanne
wiki hii akiwasilisha bungeni bajeti ya wizara yake, Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba aliliambia Bunge kuwa Serikali
itaanzisha mkoa mpya wa kipolisi katika wilaya za Kibiti, Rufiji,
Mkuranga na Mafia. Utaitwa mkoa wa kipolisi Rufiji.
0 comments:
Chapisha Maoni