Baada
ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kutoa taarifa
kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa kuanzia sasa majeruhi, mahutiti
asiyeweza kutoroka atatibiwa kwanza ndipo ashughulikie fomu ya polisi
namba 3 (PF3), Jeshi la Polisi limetolea ufafanuzi zaidi wa taarifa
hiyo.
Katika taarifa ya Waziri Nchemba alisema, “Tumeamua, majeruhi, mahututi asiyeweza kutoroka,na mtu mwenye majeraha yasiyo na utata wapewe matibabu kwanza bila PF3.”
Aliendelea kueleza zaidi kwamba, “Hatua
za kufuata PF3 zianze mara moja wakati akiendelea kupewa matibabu, hii
tunalenga kuokoa maisha yao kwanza. Utaratibu huu unajicho la karibu
kutoka kwenye vyombo vyetu vya usalama ili kubaini ukweli jeraha la
mhusika.”
Kwa
upande wa Jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wake, Msemaji wa Jeshi la
Polisi, Advera Bulimba-ACP ameeleza umma wa Watazania kwamba, fomu hiyo
ni ya lazima kwa mtu yeyote aliyepata majereha kabla ya kutibiwa na
itaendelea kutumika kwa mujibu wa sheria.
“Fomu
ya Polisi namba 3 ijulikanayo kama PF.3 hutolewa kwa mtu baada ya
Polisi kupata taarifa kutoka kwa mlalamikaji au muathirika kwa matukio
yenye madhara mwilini, ajali au matukio yenye kuleta mashaka kuhusu
vyanzo vyake kama vile kipigo, kujeruhi, ubakaji, kulawiti, kunywa sumu
na mengineyo.
“Ieleweke
wazi kwamba matumizi ya PF3 ni ya lazima na yanaendelea kama kawaida
kwa mujibu wa sheria. Fomu hiyo inapaswa kutumika katika kila aina ya
tukio tajwa hapo juu ili muathirika aweze kupata matibabu katika vitu
vya afya na hatua za kiupelelezi kwa Jeshi la Polisi ziweze kuendelea.”
Aidha, ACP Bulimba aliongeza kuwa,
“Katika mazingira mengine hali ya muathirika yaweza kuwa mbaya, hivyo
huduma za kuokoa maisha (huduma ya kwanza) inaweza kuendelea kutolewa
wakati watoa huduma wakiijulisha Polisi ili kuharakisha upatikanaji wa
PF.3”
0 comments:
Chapisha Maoni