Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetangaza rasmi kumuunga
mkono Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa Kenya utakaofanyika mwezi Agosti
mwaka huu.
Msimamo huo umetolewa jana katika mkutano wa Baraza Kuu la Chama hicho
unaofanyaki mjini Dodoma, ikiwa ni maamuzi ya Baraza hilo, na kutangazwa
rasmi na mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe.
Akizungumzia uamuzi huo, Mbowe amesema sababu kuu ya uamuzi huo ni
kugeukwa na mgombea wa muungano wa ODM Raila Odinga, ambaye chama hicho
kilikuwa kikimuunga mkono mara zote.
Mbowe amesema "Kwa muda mrefu chama chetu kimekuwa kikimuunga mkono
Raila Odinga achukue nafasi ya kuliongoza Taifa la Kenya. Mwaka 2015
ilipofika zamu yetu rafiki yetu Raila Odinga alitugeuka na kumuunga
mkono adui yetu. Sisi kama Chama, safari hii tunamuunga mkono Rais Uhuru
Kenyatta na Umoja wa vyama vinavyounda JUBILEE".
Chama hicho kinaendelea na Baraza Kuu mjini Dodoma, baada ya hapo jana
kumaliza kikao cha Kamati Kuu yake, na kimedhamiria kutoka na maamuzi
mazito kuhusu mustakabali wa taifa.
0 comments:
Chapisha Maoni