Askofu
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefunguka na kusema
Watanzania tumerogwa kwani tuna kila kitu ambacho kinaweza kutufanya
kuwa mbele kimaendeleo lakini siku zote tumekuwa nyuma.
Mchungaji
Gwajima amesema hayo leo wakati akitoa mahubiri yake kwenye kanisa lake
na kusema Watanzania wamerogwa kwani wanapenda sana maandamano na vitu
visivyo na msingi kuliko kufanya kazi, anasema Tanzania ina vitu na mali
nyingi
"Ukitaka
kuingoza Tanzania lazima uwe na moyo wa mwendawazimu maana watu wake
wamerogwa mpaka wamerogeka, ni nchi ya waliorogeka tu unaweza kwenda
kusaini mikataba ya madini, nenda kasaini mkataba wa madini Japan au
Kenya uone, sisi Tanzania Watanzania tunauza ubuyu na karanga mzungu
anabeba kila kitu, sisi tumerogwa. Tanzania ina mito mingi yenye maji
lakini maji yanakwenda tu, watu hawalimi" alisema Gwajima
Mbali
na hilo Gwajima amempa tano Rais Magufuli kwa kitendo chake cha kuzuia
makontena ya madini na kusema ni hatua nzuri na Rais ashikirie hapo hapo
"Hata
kama tulisaini mikataba ya kufa mtu sawa tu Rais ashikirie hapo hapo
hakuna kuruhusu makontena mpaka wazungu macho yao yawe mekundu, kama
hatujawa tayari kuchimba madini tuyaache kwanza, wapo wanaosema sijui
tutashitakiwa, sijui mikataba itatubana ondoka na makaratasi yako hapa
yale madini ni ya kwetu, mwanasiasa unayetaka kulia ulie tu na ufe
madini hakuna kwenda" alisema Gwajima
0 comments:
Chapisha Maoni