Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umesema kutokana na kushamili
kwa ubabe, udikteta na ung’ang’anizi wa madaraka ipo siku viongozi wa
upinzani wataondolewa kwa nguvu na aibu.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, jijini Dar
es salaam baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Utendaji
kilichokutana kutathmini ushindi wa uchaguzi.
Shaka
amesema kuwa watanzania wataendelea kuiamini CCM kwa mambo mengi,
ikiwemo kuleta uhuru na mapinduzi, sera, uongozi na utawala, kujali na
kutazama maslahi mapana kwa manufaa ya umma na pia tabia ya utii wa
sheria na kuheshimu katiba bila shuruti.
“Viongozi
ving’ang’anizi wa madaraka ya kisiasa ni hatari kukabidhiwa dhamana ya
madaraka na dola, ikitokea bahati mbaya siku moja wakapewa dhamana hiyo,
hawatapisha wengine na huo utakuwa ni mwanzo wa kutikisika misingi ya
utaifa, mshikamano na amani ya nchi,”amesema Shaka.
Aidha,
Shaka amesema kuwa inashangaza kuwaona viongozi wa kisiasa ,akiwemo
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif
wakijenga himaya ndani ya vyama vyao huku wakidaiwa kufanya ubabe katika
uongozi wao.
Hata
hivyo amesema kuwa ukandamizaji au kukosekana kwa uhuru wa mawazo
naDemokrasia ndani ya upinzani,ni kielelezo tosha kuwa viongozi wake
huimba kinadharia dhana ya demokrasia huku wakishindwa kuonyesha kwa
vitendo.