Naibu
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema kuwa Tanzania mpya yenye
matokeo chanya kwa mwaka 2017 iwapo inawezekana iwapo kila mmoja wetu
atafanya kazi kwa bidii ili kuliletea taifa maendeleo.
Ameyasema
hayo wakati wa ibaada maalum ya mkesha wa kitaifa wa mwaka mpya
uliofanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam, Dk. Tulia
amewataka watanzania kuwa na ushirikiano wa pamoja ili kufikia
maendeleo.
“Tanzania
mpya na nchi mpya yenye matokeo chanya kwa mwaka 2017 inawezekana hivyo
tushirikiane kwa pamoja na kila mmoja akifanya kazi kwa bidii, lazima
maendeleo yatapatikana tu”amesema Dk. Tulia.
Aidha, amewataka watanzania kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali ili waweze kupata maendeleo kwa haraka zaidi.