Mjumbe
wa Baraza kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg. Robert PJN Kaseko
akitambulisha vijana wenzake wa UVCCM Wilaya ya Longido aliofuatana nao
baada ya kuwasili katika kituo cha Watoto Yatima Maasai Foundation
walipokwenda kuwatembelea jana tar. 01/01/2016
*******
Jana tarehe 01/01/2017 katika kusherehekea sikukuu ya Mwaka mpya, UVCCM Wilaya ya Longido wametembelea watoto Yatima Wanaolelewa na kituo Cha Masai Foundation Kata ya Namanga wilayani humo.
*******
Jana tarehe 01/01/2017 katika kusherehekea sikukuu ya Mwaka mpya, UVCCM Wilaya ya Longido wametembelea watoto Yatima Wanaolelewa na kituo Cha Masai Foundation Kata ya Namanga wilayani humo.
Akiongea
kwa niaba ya UVCCM, Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg.
Robert PJN Kaseko ambaye pia ameongoza vijana wenzake amesema; "Sisi
kama UVCCM tunatambua Serikali yetu ina mambo mengi sana ya kufanya kwa
ajili ya Watanzania hivyo wakati mwingine sisi wenye mapenzi mema na
Nchi yetu ni vizuri kuisaidia Serikali ili kuipunguzia majukumu na kuipa
nafasi ya kufanya mambo mengine.
"Hatuwezi
kuiachia serikali peke yake ili ifanye mambo haya, Vijana huliinua na
Kulijenga Taifa hivyo Vijana ni lazima kujitoa kwa hali na mali ili
kulitumikia Taifa letu kila mmoja kwa nafasi yake.
"UVCCM
Wilaya ya Longido tunaunga juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya
Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwani kiukweli Serikali ya JPM
imejikita na imedhamiria kwa dhati kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili wananchi wake.
Ndg.
Kaseko amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la watoto waishio katika
mazingira magumu linalohusisha yatima,vibaka na watoto wa mitaani na
zipo sababu kadha wa kadha zinazochangia tatizo hili kama vile
kufululiza kwa Ugomvi kwa wanandoa katika familia hupelekea watoto
kukimbia familia zao, Ugumu wa maisha husababisha baadhi ya wazazi
kukimbia familia zao na kuacha watoto kutawanyika na kukimbilia mtaani,
Vijana wadogo kujiingiza katika Mapenzi kabla ya wakati sahihi na
mapenzi yakikolea husababisha Mimba zisizotarajiwa na kwa sababu hakuwa
na maandalizi hupelekea tatizo hili n.k
"Tunaiomba
serikali iendelee kuvisaidia vituo kwa kulea watoto yatima na waishio
katika mazingira magumu kwani nao ni binadamu kama sisi na wanahitaji
kupata haki zao za msingi kama kupewa elimu ( shule ), kuishi vizuri,
kula vizuri n.k na sisi vijana tunaahidi kushirikiana barabara na
serikali katika kutatua changamoto za wananchi wake.
"Nawashukuru
sana vijana wenzangu wa CCM Wilaya ya Longido kwa kujitoa kwa hali na
mali ili kufanikisha hili." Alihitimisha Kaseko
Vijana
wa UVCCM wilaya ya Longido wakiwa Katika picha ya pamoja wakati
wakikabidhi vitu mbalimbali kama zawadi kwa Watoto Yatima wanaolelewa na
Kituo cha Masaai Foundation Kilichopo Namanga Wilaya ya Longido.
Mjumbe
wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Longido Ndg. Tunu Lemanga akiongea baada
ya kukabidhi kiasi chaTsh. 100,000/= ikiwa ni kuanza kutimiza ahadi yake
aliyoitoa jana ya kuwakatia Bima ya Afya Watoto hao kwa Muda wa Mwaka
Mmoja.
Mjumbe
wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Robert PJN Kaseko ( Mwenye tshirt ya
Kijani ), na Vijana wengine wa UVCCM Wilaya ya Longido wakiwa katika
Picha ya Pamoja na sehemu ya Watoto yatima Walipotembelea Kituo cha
Maasai Foundation jana tar. 01/01/2017
Katibu
Hamasa wa UVCCM Mkoa wa Arusha Neema Kiusa akiteta na Watoto Yatima
wanaolelewa na Kituo hicho Maasai Foundation mara baada ya UVCCM Wilaya
ya Longido kuwatembelea na kushiriki kusherehekea pamoja na watoto hao
sikukuu ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2017.