MALKIA wa filamu na mrembo wa taji la ‘Miss Tanzania’ (2006), Wema
Sepetu, amesema atawaumbua mashoga zake wote wenye tabia za kinafiki
watakaojaribu kumsogolea kwani ameshawabaini kwa yale wanayomsema.
Wema amesema kwamba, baadhi ya mashoga zake wa karibu
wamekuwa wakimchafua kwa kusema kwa sasa hana lolote na amefulia
kiuchumi.
Alisema ameamua kukaa kimya bila kuwajibu ili kujipa muda wa
kutafakari yaliyomtokea mwaka uliopita kwani amepitia mambo mengi magumu
ingawa watu wanajidanganya kwamba amefulia wakati hakuna ukweli.
“Sijafulia na anayefikiria hivyo imekula kwake, natafakari
niliyopitia wanafiki nimeshawajua na mwaka huu atakayenisogelea sitaacha
kumpasulia ukweli kwani kuna watu wamekuwa wakinitumia kama daraja la
kupatia ustaa,” alisema Wema.